Waziri Mkuu, Mizengo Pinda SERIKALI imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi za kidini zote nchini ambazo zinaonesha nia ya dhati ya kuleta maendeleo kwa wananchi. Aidha amesema serikali inakumbuka mambo mema aliyokuwa akiyatenda Kardinali Laurean Rugambwa hasa katika elimu kwa wanafunzi wa kike. Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu Peter Pinda, wakati akitoa salaam ya serikali katika maadhimisho ya kubariki kanisa kuu la Bikira Maria wa Huruma la Jimbo la Bukoba, misa ambayo iliendeshwa na Mwadhama Emmanuel Kardinali Wamala wa Jimbo kuu la Kampala nchini Uganda. Alisema kutokana na Kardinali huyo kutumia vizuri misaada ya wahisani ndiyo ilimwezesha kujenga shule ya sekondari ya Rugambwa ambayo imekuwa chachu kubwa hapa nyingi kwa kufundisha watoto wengi wa kike ambao hadi sasa baadhi yao ni Mawaziri na wengi wakishikilia nafasi mbali mbali serikalini. Alisema katika historia yake na maisha yake alipenda elimu, ndiyo maana miaka ya 50 aliweza kuanzisha chama cha vijana kwa jili ya kuwaweka pamoja vijana katika ulimwegu wa kusoma ambapo kwa wale waliokuwa na akili waliweza kupelekwa nje ya nchi kuongeza elimu ya juu. Alisema katika miaka hiyo, serikali ya Tanzania ilikuwa bado changa, lakini aliweza kuisaidia serikali katika kuinua sekta ya elimu. “Katika kupigania maendeleo ya wananchi hakuishia katika elimu tu, bali aliweza kuanzisha huduma za jamii, kama hospitali ya Rubya pamoja na vituo mbali mbali licha ya kuwa alipenda huduma za kiroho lakini hata za kijamii pia” alisema Waziri Pinda. Alisema kwa vitendo alikidhi mahitaji ya wananchi, na hivyo sifa zake hazitasahulika hapa nchini. Aidha Waziri huyo aliupongeza kanisa katoliki jimbo la Bukoba kwa kujenga kanisa ambalo linavutia na inatia imani ambapo itaweza kuwakusanya waumini pamoja kumwabudu Mungu. Alisema kutokana na kanisa hilo,imani yake ni matumizi mazuri ya kanisa hilo ambalo litazaa matunda ya waumini na jamii walio wema na waadilifu, siku hadi siku, kwani serikali inawategemea wao kujenga taifa lenye waungwana na wenye upendo. Hali kadhalika alimpongeza Askofu wa Jimbo la Bukoba, Nestory Timanywa kwa kuonesha kuendeleza ndoto na vitendo vya Kardinali Rugambwa ya kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Alisema kwa hadi sasa kuna shule sita za msingi tano sekondari, chuo kimoja cha ualimu, vyuo vinne vya afya , yote hayo michango kwa ajili ya kusaidia serikali kuendeleza taifa. Alisema Kardinali Rugambwa alikuwa ni miongozi mwa viongozi 130 wa juu kabisa ulimwenguni wa kanisa katoliki wa kumshauri Papa Mtakatifu. |
Pata habari moto moto kila siku, kwa Mawasiliano zaidi piga Simu Na. 0755 856991/ 0712 992434 Email:-theonestinajuma@yahoo.com/rorya.09@gmail.com
Monday, October 8, 2012
Watanzania watakiwa kumuenzi Kardinali Rugambwa-Waziri Pinda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment