Na Theonestina Juma, Bukoba
MAJAMBAZI wapatao watatu waliokuwa na visu na
mapanga wamewavamia wavuvi watatu na kumuua mmoja wao kikatili na kisha
kuwapora mali zao zote ikiwemo samaki tani moja katika kisiwa cha Gozba ndani
ya ziwa Victoria upande wa Wilaya ya Rorya.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 3,
mwaka huu saa 5 asubuhi katika kisichwa cha Gozba upande wa Wilayani Rorya
Mkoani Mara ikiwa ni siku yao nne ya wakiwa kisiwani humo wakitega
samaki.
Mvuvi aliyeuawa kikatili kisiwani humo, ni Bw. Godfrey Ogwanda (24)
maarufu kwa jina la Yambo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka
Katika kijiji cha Bubombi wilayani Rorya, Kaka wa marehemu, Bw. Guka Ogwanda
alisema kaka yake wakiwa na wavuvi wenzake wawili walivamia na majambazi hayo,
ziwani wakitega samaki ambapo Bw. Ogwanda aliuuawa kwa kundungwa kisu
shingoni.
Alisema kabla ya majambazi hayo hawajamuua, Bw. Ogwanda, waliwaona
kama wavuvi wenzao , licha ya kuwa walikuwa hawafahamu kabisa, ambapo walileta
mtumbwi wao karibu na ya kwao wakiwa hawajui lengo lao.
Alisema mmoja wa
wamajambazi hao, waliwaomba kisu cha kutengenezea samaki, ambapo akina kaka yake
waliwahoji, wao kama wavuvi wanawezaje kuja kisiwani kuvua sakami bila kuwa na
kisu cha kutengenezea sakaki?
Hata hivyo, inadaiwa kuwa watu hao waliwapatia
kisu chao walichokuwa nacho, na baadaye majambazi hayo kuwabadilikia na
kuwavamia, na kuanza kuwatosa majini na kisha kuchukua mtumbwi wao na
kuunganisha na wa kwao na kufunga kwa kamba.
Baada ya kitendo hicho
majambazi hayo, waliwaingiza wavuvi waliowatosa majini kwenye mtumbwi wao na
kuanza kuchukua mbao walizokuwa nazo ambazo huwa wanatembea nazo ndani ya
mtumbwi kwa ajili ya kulalia nyakati za usiku na kuwaamuru kulala kifudi fudi na
kuwafunika na mbao hizo na kuwaamwagia barafu waliazokuwa nazo juu ya mbao hizo.
Baada yakitendo hicho, walimdunga kisu Bw. Ogwanda shingoni urefu wa inchi
mbili na nusu upande wa mkono wa kulia, na kuanguka chini, na wao majambazi
kuanza kupakia samaki za wavuvi hao kwenye mtumbwi wao.
Alisema majambazi
hayo waliwapora mafula ya dizeli lita 60 na injini ya mtumbwi wao waliokuwa
nayo na kuondoka navyo ambapo Bw. Ogwanda alifia papo hapo kutokana na kuvuja
damu nyingi.
Alisema kwa kawaida wavuvi kutoka katika kisiwa cha Sota
Shirati, hulazimika kutembea na vyakula vyao, wakati wakisafiri kwenda kutega
samaki kutokana na sehemu wanakoenda ni mbali na huwachukua siku nne hadi wiki
wakitega samaki.
Halikadhalika wavuvi hao hawatembei na silaha aina yoyote
kutokana na kuwepo kwa ukaguzi wanaofanyiwa mfano kama sehemu ya Migingo upande
wa Uganda polisi walioko maeneo hayo huwakagua.
Aidha wavuvi hao hulazimika
kutembea na kisu kwa jili ya kutengezea samaki pindi inapoonekana kutaka
kuharibika, na pia hukitumia wakati wa kupika.
Hata hivyo, gazeti hili
likizungumza na Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Tarime/ Rorya, Bw. Zakaria
Sebastian alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa hajapata taarifa kamili
juu yatukio hilo kutoka katika kituo kidogo cha Polisi cha Shirati.
“Tukio
hilo lipo, lakini hadi sasa bado sijapata taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa
kituo kidogo cha Shirati, na tatizo kubwa kati yao na hapa ni
mawasiliano”alisema kamanda Sebastian.
No comments:
Post a Comment