Wednesday, October 31, 2012

HUZUNI, Picha za watoto 7 waliouawa na bomu Karagwe

 

Miili ya watoto watatu waliouawa na bomu papo hapo, wakiwa wamefunikwa kwa khanga wakisubiri kupekwa katika hospitali ya Nyakahanga katika chumba cha kuhifadhia maiti.

Na Theonestina Juma, Karagwe
WATOTO watano wakiwemo wanne wa familia moja Wilayani Karagwe Mkoani Kagera wamefariki dunia kwa kulipukiwa na  bomu la kutupwa kwa mkono wakati wakilichezea kwa zamu huku wengine wakichambua vyuma chakavu kwa ajili yha kwenda kuviuza.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea  Oktoba 30, mwaka huu saa 4 asubuhi katika kijiji cha Ihanda na Kata ya Ihanda katika  kitongoji cha Rugarama wilayani hapa.
Watoto waliouawa na bomu hilo wamejulikana kuwa ni pamoja na Fenius Frank miaka mitatu na nusu, Faraja Frank mwaka mmoja na miezi mitatu,na Skatus Kamali (15) wote ni watoto wa familia moja na hao wakubwa wamehitimu elimu ya msingi mwaka huu.
Wengine ni pamoja na Nelson Alfons (14),Edger Gidion na Eradius Robert (17) amejeruhiwa vibaya na amelazwa katika hospitali ya Nyakahanga wilayani humo.
Hata hivyo, mtoto ERADIUS aliyejeruhiwa vibaya huku jnicho lake moja likitoka ndiye serikali ya wilayani humo inamtegemea kama atapona ndiye ataweza kutoa maelezo jinsi bomu hilo lilivyolipuka,lakini hali yake ni mbaya na amelazwa katika hospitali teule ya wilaya Nyakahanga.
Tukio hilo la kusitisha na lililovutia hisia za viongozi wa  wakuu wa wilaya za Karagwe na Kyerwa, waliokuwa wakihudhuria katika kikao cha baraza la madiwani walilazimika kusitisha ushiriki na kukimbia katika eneo la tukio.
Akingumza kwa huzuni katika eneo la tukio hilo baba mzazi wa watoto wanne wa familia moja, Bw.Frank Robert (35) alisema watoto hao walikusanya vyuma chakavu kijijini hapo na kuvilundika nyumbani kwake.
Alisema kati ya vyuma hivyo aliona kitu mfano wa  kibuyu lakini hakuweza kukifuatilia ili kuona ni nini.
"Kuna kitu kama kibuyu nilikiona kwenye vyuma vyao walivyovikusanya hapa,lakini sikukitilia manani kwani si mara yao ya kwanza kukusanya vyuma hivyo kwa ajili ya kuwauzia wafanyabishara wanaotoka mjini Bukoba, Mwanza na Uganda"alisema kwahuzuni.
Hata hivyo, watpoto hao wanaelezwa kuwa walikuwa wakilichezea bomu hilo tangu jana ambapo ilipifika usiku kutokana na baba yao hakulitilia maanani hakuweza kufuatilia ni wapi walikolihifadhi.
Halikadhalika kulipokucha watoto hao waliendelea kulichezea hadi ilipolipuka.
Kwa upande wa Mshauri wa Mgambo wa Jeshi la wananchi Wilayani hapa,Bw.Mukama Sadock pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Benedict Kitenga wakizungumza katika eneo la tukio walithibitisha kuwa hilo ni bomu la kurushwa kwa mkono unaojulikana kama 'Decensive handgrunet'.
Mkuu huyo ambaye pia ni mtaalamu wa kutegua mabomu na mhandisi alisema huenda mtoto mmoja alijaribu kuvuta kamba au pini ya bomu hilo kwa kutaka kuona kilichomo ndani na ndipo likalipuka.
Kutokana na hali hiyo ametoa tahadhari kwa wakazi wa wilayani hapa kuwa makini na eneo hilo kutokana na watu kutoka mataifa tofauti wanaoenda eneo hilo kutokana na kuwa na kiwanda cha kahawa cha Kagera Estate kinachomilikiwa na mmoja wa Mbunge wa mkoani Kagera.
Aidha amewataka kuchukua tahadhari kwa kitu chochote ambapo wanakitilia shaka.
Hata hivyo, kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Bi. Darry Rwegasira amewataka wananchi kupuuza ujumbe mfupi wa simu uonasambazwa kwa wananchi kuwa hilo ni hujuma, ambao umefanywa na moja ya nchi jirani.
Miili ya watoto hao yamehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Nyakahanga ambapo baadhi yao wanatarajiwa kuzikwa leo.
mwisho

Kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kyerwa, Mhandisi, Benedict Kitega wa kati kati aliyewekewa kinasa sauti wakiwa katika eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment