Na Theonestina Juma,
Bukoba
MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Bukoba, aliyetakiwa kuanza kufanya mtihani wake wa mwisho jana, amezuiliwa kufanya mtihani huo, kutokana na kuwa na mimba ya miezi tisa.
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Agnes Vedasto (16-18) mwenye namba ya mtihani S.0304/0003 amekumbwa na tatizo hilo baada ya jana kuwasili shuleni hapo kwa lengo la kutaka kufanya mitihani hiyo.
Hata hivyo, kabla ya kuingia darasa kuanza kufanya mtihani huo, aliingia Afisa elimu Taalum, Bi. Christina Shadrack na Afisa elimu Vifaa na takwimu wa Manispaa ya Bukoba, Bw. Wandele Pamba wakiwa wanasambaza vifaa vya mtihani kutokana na shule hiyo ndicho kilikuwa kituo cha mwisho, waliuzwa na Mkuu wa shule hiyo, Bw. Deus Gaspar kama mwanafunzi huyo anaweza kuruhusiwa kufanya mtihani.
Mkuu huyo wa shule hiyo Bw. Gasper alisema alilazimika kumrudisha nyumbani mwanafunzi huyo ambapo alisema kuwa miezi mitatu ya mwishoni mwanafunzi huyo alikuwa hajaonekana shuleni hapo.
Bw. Gasper alisema uongozi wa shule hiyo ulijua kuwa mwanafunzi huyo ni mjamzito, ambapo aliitwa mzazi akakiri kuwa mwanae ni mjamzito.
Hata hivyo, kutokana na tayari jina lake lilishapelekwa baraza la mtihani, lakini lilirudi na wanafunzi wenzake wakamtaarifu juu ya hilo na yeye kuamua kufika shuleni hapo siku ya kuanza mtihani akiwa na vifaa vya shule, amevaa sare huku tumbo likiwa limetangulia.
“ Uongozi wa shule ulijua kuwa mwanafunzi huyo ni mjamzito, na tulishamrudisha nyumbani, lakini tayari jina lake lilishaenda baraza la mtihani na limerudi… na wanafunzi wenzake wamemwambia kuwa jina lake limo kwenye orodha na hivyo naye amelazimika kuja shule kufanya mtihani”alisema mkuu wa shule hiyo.
Hata hivyo, kwa upande wa Afisa elimu wa Manispaa ya Bukoba, Simon Mwombeki alisema kwa mujibu wa sheria ya elimu namba 25 ni kosa mwanafunzi kupata ujauzito akiwa shule, kuoa wala kuolewa, hivyo mwanafunzi huyo tayari amekosa sifa.
Afisa huyo alisema, mama yake mzazi mwanafunzi huyo ambaye hakutaja jina lake, jana alifika ofisini kwake kumwomba mwanae aruhusiwe kufanya mtihani huo lakini haikuwezekana.
Alisema kulingana na maelezo ya mama mzazi wa mwanafunzi huyo, mwanae huyo anatarajiwa kujifungua kati ya tarehe 25 au 26 mwezi huu.
Jumla ya wanafunzi wanaofanya mtihani huo katika shule ya sekondari ya Bukoba ni 223 badala ya 224.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment