Gari lililobeba masalia ya Kardinali Rugambwa likiwa limepaki mbele ya kanisa hilo muda mfupi baada ya kutoka Parokia ya Kashozi. |
Watu walioandaliwa maalum kushughulikia kuhamisha masalia yake wakijiandaa kuondoa jeneza lake ndani ya gari tayari kuingizwa ndani ya Kanisa Kuu kwa maziko |
Gari hilo likingia katika viwanja vya Kanisa hilo likiwa limebeba jeneza la masalia ya Kardinali Rugambwa
Hawa ni baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule yake ya sekondari ya Rugambwa alioijenga na kutaifishwa na serikali nao walikuwa katika maandamano ya kuupokea mwili huo kwa maziko
Gwaride la shule ya msingi ya mchipuo ya Kiingereza cha Kolping Aldof inayomilikiwa na ksani Katoliki Jimbo la Bukoba wakifanya vitu vyao, baada ya kupokea maandamano ya kusindikiza masalia ya Kardinali Rugambwa
Jeneza lililo na masalia likiwa mbele ya Kanisa la Kashozi tayari kuombewa kwa maziko
Hata watu kutoka nj ya nchi nao hawakukosekana hii ni ngoma kutoka nchi jirani ya Burundi.
Waziri wa Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Zipora Pangani nao walikuwa ni miongoni mwa viongozi wa serikali waliohudhuria katika misa ya kuhamisha masalia ya Kardinali Rugambwa
No comments:
Post a Comment