TAARIFA kutoka mkoani
Iringa ambazo zimeufikia mtandao huu
asubuhi hii zinadai kuwa aliyekuwa mweka hazina wa chama cha waandishi wa habari
mkoa wa Iringa(IPC) na mwandishi wa magazeti ya NIpashe mkoa wa Iringa Vichky
Macha (pichani) amefariki dunia asubuhi hii.
Vicky Macha kabla ya kifo chake alikuwa
amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa akisumbulia ugonjwa wa Maralia na
kulazwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa kabla ya leo asubuhi hii kufariki
dunia.
Vicky Macha katika uhai wake alipata kufanya kazi kwa karibu na
marehemu Daudi Mwangosi ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa (IPC) na hata siku
aliyefariki dunia Vicky Macha kama mweka hazina wa IPC mara baada ya kumweleza
juu ya kifo cha Mwangosi alipoteza fahamu kwa muda katika ofisi za IPC
. Hata hivyo
kutokana na siku ya tukio viongozi mkuu nilikuwa ni mimi Francis Godwin ambaye
nilikuwa ni naibu katibu mkuu wa IPC kwa kushirikiana na vema na Vicky tuliweza
kujikaza na kuhakikisha mambo yanakwenda vema japo mara kwa mara mwenzake
alikuwa akiishiwa nguvu na mimi pia nikiishiwa nguvu na kujikuta tukibembelezana
na kujikaza.
Rais wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari
Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya (kulia) akikabidhi mchango wa rambi rambi ya kifo
cha Mwangosi kwa makamu mwenyekiti wa IPC Francis Godwin kutoka kwa vilabu mbali
mbali vya wanabari nchini kwa ajili ya kifo hicho , katikati ni marehemu Vicky
Macha akilia kwa uchungu na kushoto ni katibu mtendaji wa IPC Frank
Leonard.
Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea hapa
jambo kwa sasa naweza kusema Bwana ametoa na
Bwana ametwaa jina lake na lihimidiwe milele
Chanzo Francis
Godwin |
No comments:
Post a Comment