Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Liberatus Barlow ameuawa na majambazi usiku wa kuamuakia leo katika maeneo ya Kitangiri Jijini Mwanza.
Habari zilizopatikana kutoka jijini humo na kuthibitishwa na IGP Said Mwema zinasema kuwa Kamanda Barlow aliuawa na majambazi wakati akitoka kumsindikiza dada yake baada ya kuhudhuria kikao cha harusi.
Hata hivyo habari zaidi zinasema kuwa tayari mwalimu mmoja aliyejulikana kwa jina la Doroth anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa ajili ya kulisaidia katika uchunguzi wa watu waliomuua kamanda huyo kwa kummiminia risasi .
Mwalimu Doroth ndiye inasemekana kuwa alikuwa dada yake aliyetoka kumsindikiza mufa mufupi kabla ya kuuawa.
Kamanda Barlow aliuawa usiku saa tisa.
No comments:
Post a Comment