Sunday, October 7, 2012

Mvua ilivyoharibu shamrashamra ya wakatoliki Bukoba wakati wa kutabaruku kanisa Kuu alimozikwa Kardinali Rugambwa

 Hali halisi ilivyokuwa wakati wa kuanza kwa misa ya kutabaruku Kanisa Kuu katoliki la Bukoba, alimozikwa masalia ya Kardinali Laurean Rugambwa.Mvua kubwa ilioambatana ilipiga hadi waumini waliokaa nje walishindwa sehemu pa kujikinga
 Hapa watu wakiwa wamejikusanua makundi makundi kuchangia miavuli iliokuwepo,mvua ilikuwa kumbwa hata mtu aliyekuwa mbele yako haikuwa rahisi kumuona
 Hapa waumini wakiwa wamejikusanya mbele ya lanho kuu la kuingilia kanisa kuu lililozinduliwa leo baada ya maziko ya Kardinali Rugambwa, wakiwaomba walinzi waliokuwa wakilinda wawafungulie bila huruma, hata haya walifunga geti na waumini kushindwa sehemu pa kupita kuingia kanisani.
 Yaani hata mahema yaliojengwa kwa ajili ya kukaa watu hapoakukalika wakati wa bonge la mvua ilipopiga leo.
Watu walijaribu hata kujikinga chini ya miti lakini walioloa chapa chapa chapa

No comments:

Post a Comment