Na Theonestina Juma, Bukoba
MWANAFUNZI Stella Charles (23) wa kidato cha nne
katika shule ya sekondari Kagemu, nusura juzi ajifungue katika chumba
cha mtihani baada ya kushikwa na uchungu wa uzazi.
Tukio hilo la aina yake
ambalo limekuja siku chache baada ya mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule
ya sekondari ya Bukoba, Agnes Vedasto (16-17) kuzujiliwa kufanya mtihani
kutokana na kuwa na mimba ya miezi tisa.
Mwanafunzi huyo, Charles alijifungua
mtoto wa kike Oktoba 12, mwaka huu saa 2.30 usiku kwa njia ya upasuaji na
amelazwa katika wodi ya wazazi namba 9 katika chumba cha waliojifungua kwa
upasuaji hali yake ikiwa inaendelea vizuri, kutokana na awali alikuwa
akikabiliwa na ugonjwa wa kifafa cha uzazi.
Hayo yamebainika leo baada ya
waandishi wa habari kufika hospitalini hapo kumjulia hli baada ya uongozi wa
hospitali ya Mkoa Kagera kushindwa kutoa ushirikiano kwa wandishi wa habari
waliokuwa wkaifuatilia suala hilo.
Waandishi wa habari walilazimika kujifanya
kama wanaoenda kuwaona wagonjwa jana (leo) saa 7.00 ikiwa ndiyo muda wa
kuwapelekea wagonjwa chakula katika hospitali ya mkoa Kagera.
Mwanafunzi huyo
akizungumza na waandishi wa habari bila kujua anazungumza na akina nani, alisema
alikuwa akijua wazi kuwa ni mjamzito, hata baadhi ya walimu wake walijua lakini
walimtaka ajikaze ili afanye mtihani wake wa mwisho.
Alisema siku ambayo
anashikwa na uchungu, alisikia kama anaumwa jino, ambapo akiwa katika mtihani wa
vitendo (Practical) somo la Biologia saa 5 asubuhi, alianguka chini na kupoteza
fahamu.
Alisema kutokana na hali hiyo, alipewa huduma ya kwanza ikiwa ni
pamoja na kupewa dawa aina ya panadol ambapo alipopata tena ahueni na kurudi
kuendelea na practical hiyo,alidondoka chini na uongozi wa shule kulazimika
kukimbikiza katika hospitali ya mkoa kwa kutumia gari la shule.
Alisema
“tangu asubuhi naingia kwenye chumba cha kufanya mtihani wa pratical, nilikuwa
sijikii vizuri, nilisikia kama jino linaniuma na sikutegemea kujifungua wiki
hii, wala kujifungulia hapa, mimi nilitegemea kwenda kujifungulia nyumbani
lakini nimeshangaa, lakini namshukuru Mungu nimemaliza mtihani
wangu”alisema.
Akizungumzia mategemeo yake ya mbeleni ni kuwa mwanasheria,
licha ya kuwa mtihani wake wa pratical hakuweza kumaliza.
Hata hivyo,
mwanafunzi huyo alipofikishwa hospitalin I hapo, alipopimwa alikutwa akiwa
anaumwa uchungu lakini mtoto huyo amezaliwa kabla ya kutimiza miezi tisa kamili
kwani alibakiwa na takribani wiki moja kulingana na maelezo aliopewa na
madaktari.
Mwanafunzi ambaye hana mama zaidi ya baba yake ambaye anaishi
wilayani Sengerema Mkoani Mwanza na anakabiliwa na ugonjwa wa kiharusi alikuwa
akiishi na kaka yake Bw. John Charles tangu utotoni na kwamba ndiye alikuwa
akimsomesha lakini wakati akikaribia kumaliza elimu hiyo alikorofishana na wifi
yake na kulazimika kuhamia kwa mtu mwingine.
Alisema mke aliyemlea ni mke wa
kwanza wa kaka yake, ambapo walikorofishana na kaka yake huyo na Bw. John na
kukimbia na Bw. John akaamua kkuoa mke mwingine, ambaye ndiye alimfukuza kwake
baada ya kumleta mdogo wake wa kike ambaye hasomi.
Alisema kutokana na hali
hiyo, mwanafunzi mmoja anayesoma shule ya sekondari ya Bukoba na anahitimu elimu
yake ya sekondari mwaka huu, aliyemtaja kwa jina la Thobias, Charles alilazimika
kwenda kwa baba yake mzazi kumwombea akae hapo kutokana kujua matatizo
ayanayomkabili na ikizingatiwa kuwa wote ni ni wasukuma, ambapo baba yake
Thobias aliridhia.
Hata hivyo kwao Thobias ambako amekaa takribani miezi
mitatu, hadi anafikia hatua ya kujifungua, hakuna mtu alayejua kama ni
mjamzito.
Hata hivyo, baadhi ya wanawake wawili ambao waandishi wa habari
waliwakuta wakumhudumia mwanafunzi huyo,wakizungumza na wandishi wao bila kuwa
ni akina nani aliyejitambulisha kwa jina la Grace Leonard mkazi wa kijiji cha
Kabale alisema mwanafunzi huyo, alifikishwa hospitalini hapo akiwa
hajitambui.
“Stella aliletwa hapa akiwa hajitambui, lakini tunamshukuru
Mungu, amejifungua mtoto wake wa kike, lakini kwa njia ya upasuaji, na alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa lakini kadri siku zinazvyokwenda hali yake
inazidi kuimarika”alisema Bi. Grace.
Grace alisema yeye kutokana na kuwa na
uzoefu na wanawake wenye mimba, alimhisi kuwa mjamzito kutokana na miguu yake
kuvimba lakini hakuweza kumuliizia kutokana na mwanafunzi huyo alikuwa kijisomea
kwa bidii pindi alipomaliza shughuli za nyumbani.
Alisema mwanafunzi huyo,
alikuwa amepewa sehemu ya kukaa nyumbani kwao kwa takribani miezi mitatu sasa,
baada ya kufukuzwa na wifi yake mke wa kaka yake aliyemtaja kwa jina la John
Charles.
Gazeti hili lilishudhia wanawake wengi wakiingia katika chumba
hicho, kumpa hongera huku wengine wakilazimika kununulia khanga kwa ajili ya
madaso ya mtoto kiutokana na kutokuwa na msaada wowote.
Hata hivyo,
mwanafunzi huyo alipoulizwa juu ya baba mtoto huyo, alisema kuwa anafanya kazi
katika Kampuni ya basi la Mombasa raha, ambapo hakuwa tayari kumtaja jina lake.
Tukio
hilo limethibitishwa na Afisa elimu Sekondari wa Manispaa ya Bukoba, Bw. Simon
Mwombeki ambapo hata hivyo alisema kuwa mwanafunzi huyo amelazwa lakini taarifa
ya kujifungua hajapata, kulingana na maelezo aliopewa na Mkuu wa shule hiyo
aliyemtaja kwa jina la Thadeus Lungu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment