Hapa si kwamba ilifika muda wa kusimama wakati misa ikiendelea ndani la hasha, bali sababu ya mvua kubwa ilioambatana na upepo uliwashinda waumini hawa kukaa, ikizingatiwa kuwa hawakuwa ma viti zaidi ya kuandaliwa majani ya kukalia kulingana na mila za Uhayani.
Upepo uliangusha hadi mahema yalioandaliwa, na waumini wakihangaika ni wapi pa kujihifadhi, huku wengine wakidiriki kukijinga chini ya miti kama inavyoonekana
Angalia mwenyewe
Hata sehemu hii ilioandaliwa kwa ajili ya kuwekea mitambo mbali mbali iliweza kuangushwa chini na upepo, pamoja na nguzo ya chuma hicho kinachoonekana kilichimbiwa chini na kujengelewa kwa sementi lakini yanaonekana ilikuwa chini ya kiwango.
Waliokuwa na kiti walijaribu kikutumia kukinga mvua, cha ajabu waumini hawa walikuwa mbele ya milango ya kuingilia kanisani, lakini walizuiwa kwani waliokuwemo ndani ni wale waliokuwa maalum tu, na waumini hawakuruhusiwa kusimama wakiwa ndani.
No comments:
Post a Comment