Friday, October 5, 2012

Maziko rasmi ya Kardinali Rugambwa, vyumba vimejaa,wageni waombewa kwa wasamaria wema kuwahifadhi-Kilaini

Na Theonestina Juma, Bukoba
MAANDALIZI ya kuzika rasmi masalia ya Kardinali Laurean Rugambwa yamekamika kwa asilimia kumbapo kwa sasa hofu kubwa iliopo ni mji wa Bukoba kukabiliwa na upungufu wa mkubwa wa nyumba za kulala wageni ambapo baadhi yao wameanza kuhifadhiwa kwa watu binafsi waliojitolea.
Halikadhalika katika sherehe hizo, Waziri Mkuu,Mizengo Pinda ndiye anatarajiwa kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete ambapo anatarajiwa kuwasilia mjini Bukoba kesho lasiri.
Hayo yamesemwa na Askofu Methodius Kilaini wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu leo, alipotaka kujua maandalizi yamefika wapi, ambapo maziko ya Kardinali Rugambwa yanatarajiwa kufanyika  rasmi Oktoba 6, mwaka huu mjini Bukoba.
Askofu Kilaini alisema, hadi hivi sasa maandalizi yanaaelekea kukamilika, na kwamba kitu kilichobaki ni shughuli za upambaji, lakini wanakabiliwa na sehemu pa kuwalaza wageni kutokana na watu wanazidi  wengi.
“Maandalizi ni kama yamekamilika kitu kilichobaki ni upambaji ndicho kinachoendelea,lakini kumeibuka tatizo kubwa la vyumba vya kulala wageni, vimepungua kwa kiasi kikubwa, hadi imefikia hatua ya kuomba watu  binafsi watupe hifadhi kwa ajili ya wageni hao ambapo hata maeneo hayo nayo yameshajaa”alisema.
“Kuna watu wameanza kujitokeza kutupa nafasi katika nyumba zao binfasi kwa ajili ya kulala wageni wetu ambao wanazidi kuongezeka kuhudhuria katika maziko hayo ya Kardinali Rugambwa hapo kesho, katika Kanisa kuu la Bikira Maria wa Huruma  mjini Bukoba”aliongeza.
Alisema watu hao waliojitolea kutoka nafasi katika nyumba zao, hawatozi ambapo wageni hao wanalala bure bila kulipa.
Kuhusu idadi ya maaskofu ambao tayari wameshawasili mjini Bukoba, Askofu Kilaini alisema kuwa hadi saa 6 mchana walishafika maaskofu 12 bila kutaja majimbo na nchi wanakotoka.
Aidha alipoulizwa kuhusiana na Kardinali Emmanuel Wamala kutoka Nchini Uganda kama ameshawasili, alisema kuwa tayari wameshafika mpakani Mutukula, wanakuja kwa njia ya gari.
“Kardinali Wamala na msafara wake tayari wameshafika mpakani Mutukula, wanakuja hivyo muda mfupi tu atakuwa ameshawasili”alibainisha.
Kuhusu wageni wa kitaifa ambao wameshawasili, alisema kuwa hadi hivi sasa bado lakini wanatarajia kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndiye anayetarajiwa kuwasili mkoani hapa kesho saa 9 alasiri, ambapo ataondoka Oktoba 7 saa 10 baada ya misa ya kubariki kanisa hilo.
Hata hivyo, kwa upande wa Mkuu wa mkoa Kagera, Kanali Fabian Massawe akizungumza na gazeti hili lililotaka kujua hali ya usalama uko vipi kulingana na ugeni uliopo kutoka ndani na nje ya nchi, alisema kuwa askari wamesambazwa kila kona ya  mjini hapa hata Parokia ya Kashozi kwa ajili ya kulinda usalama.
“Nawahakikishia wananchi kuwa hali ya usalama uko shwari, wao wajitokeze kwa uwingi kumzika masalia ya Kardinali Rugambwa.
Hata hivyo alipoulizwa kama wameongeza askari kutoka nje ya mkoa Kagera, alisema kuwa wameweza kutumia askari wa mkoani hapa pekee na hivyo ulinzi umeimarishwa.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kutokana na nyumba za wageni kujaa, mjini Bukoba asilimia kubwa ya wageni wamelazimika kulala katika wilaya za Muleba na Missenyi
Katika maziko hayo katika historia ya Kanisa Katoliki, hayatahudhuriwa na Kardinali wa Tanzania, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kutokana na kuwa nchini Roma kikazi.

No comments:

Post a Comment