Miili ya watoto watatu waliouawa na bomu papo hapo, wakiwa wamefunikwa kwa khanga wakisubiri kupekwa katika hospitali ya Nyakahanga katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Na Theonestina Juma, Karagwe
WATOTO watano wakiwemo
wanne wa familia moja Wilayani Karagwe Mkoani Kagera wamefariki dunia kwa
kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono wakati
wakilichezea kwa zamu huku wengine wakichambua vyuma chakavu kwa ajili yha kwenda kuviuza.
Tukio hilo
la kusikitisha limetokea Oktoba 30,
mwaka huu saa 4 asubuhi katika kijiji cha Ihanda na Kata ya Ihanda katika kitongoji cha Rugarama wilayani hapa.
Watoto waliouawa
na bomu hilo wamejulikana kuwa ni pamoja na Fenius Frank miaka mitatu na nusu,
Faraja Frank mwaka mmoja na miezi mitatu,na Skatus Kamali (15)
wote ni watoto wa familia moja na hao wakubwa wamehitimu elimu ya msingi mwaka huu.
Wengine ni
pamoja na Nelson Alfons (14),Edger Gidion na Eradius Robert (17) amejeruhiwa vibaya na amelazwa katika hospitali ya Nyakahanga wilayani humo.
Hata hivyo, mtoto
ERADIUS aliyejeruhiwa vibaya huku jnicho lake moja likitoka ndiye serikali ya wilayani humo inamtegemea kama
atapona ndiye ataweza kutoa maelezo jinsi bomu hilo lilivyolipuka,lakini hali yake ni mbaya na amelazwa katika hospitali teule ya wilaya Nyakahanga.
Tukio hilo
la kusitisha na lililovutia hisia za viongozi wa wakuu wa wilaya za Karagwe
na Kyerwa, waliokuwa wakihudhuria katika kikao cha baraza la madiwani
walilazimika kusitisha ushiriki na kukimbia katika eneo la tukio.
Akingumza
kwa huzuni katika eneo la tukio hilo baba mzazi wa watoto wanne wa familia
moja, Bw.Frank Robert (35) alisema watoto hao walikusanya vyuma chakavu kijijini
hapo na kuvilundika nyumbani kwake.
Alisema kati
ya vyuma hivyo aliona kitu mfano wa kibuyu lakini hakuweza kukifuatilia
ili kuona ni nini.
"Kuna
kitu kama kibuyu nilikiona kwenye vyuma vyao walivyovikusanya hapa,lakini
sikukitilia manani kwani si mara yao ya kwanza kukusanya vyuma hivyo kwa ajili
ya kuwauzia wafanyabishara wanaotoka mjini Bukoba, Mwanza na
Uganda"alisema kwahuzuni.
Hata hivyo,
watpoto hao wanaelezwa kuwa walikuwa wakilichezea bomu hilo tangu jana ambapo
ilipifika usiku kutokana na baba yao hakulitilia maanani hakuweza kufuatilia ni
wapi walikolihifadhi.
Halikadhalika
kulipokucha watoto hao waliendelea kulichezea hadi ilipolipuka.
Kwa upande
wa Mshauri wa Mgambo wa Jeshi la wananchi Wilayani hapa,Bw.Mukama Sadock pamoja
na Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Benedict Kitenga wakizungumza katika eneo la tukio
walithibitisha kuwa hilo ni bomu la kurushwa kwa mkono unaojulikana kama
'Decensive handgrunet'.
Mkuu huyo
ambaye pia ni mtaalamu wa kutegua mabomu na mhandisi alisema huenda mtoto mmoja
alijaribu kuvuta kamba au pini ya bomu hilo kwa kutaka kuona kilichomo ndani na
ndipo likalipuka.
Kutokana na
hali hiyo ametoa tahadhari kwa wakazi wa wilayani hapa kuwa makini na eneo hilo
kutokana na watu kutoka mataifa tofauti wanaoenda eneo hilo kutokana na kuwa na
kiwanda cha kahawa cha Kagera Estate kinachomilikiwa na mmoja wa Mbunge wa
mkoani Kagera.
Aidha amewataka
kuchukua tahadhari kwa kitu chochote ambapo wanakitilia shaka.
Hata hivyo,
kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Karagwe, Bi. Darry Rwegasira amewataka wananchi
kupuuza ujumbe mfupi wa simu uonasambazwa kwa wananchi kuwa hilo ni hujuma,
ambao umefanywa na moja ya nchi jirani.
Miili ya
watoto hao yamehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Nyakahanga ambapo baadhi
yao wanatarajiwa kuzikwa leo.
mwisho
Kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kyerwa, Mhandisi, Benedict Kitega wa kati kati aliyewekewa kinasa sauti wakiwa katika eneo la tukio.