Na Theonestina
Juma, Uganda
KUTOKANA na baadhi ya viongozi wa nchini Uganda kudai kuwa hawajisikii vizuri Kiswahili kutumika katika mazungumzo ya Ushirikiano wa Jumiya ya Afrika Mashariki katika mkutano uliotangulia juzi iliwalazimu kukaa kimya baada ya viongozi kutoka Tanzania kukitumia lugha hiyo kuanzia mwanzo hadi mwisho wa majadiliano.
Hayo yalibainika Oktoba 24, mwaka 2011 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Malaba wilaya ya Rakai nchini Uganda, uliohudhuriwa na Naibu wa Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) nchini humo, Bw. Eriya Kategaya ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, pamoja na ujumbe kutoka Tanzania ulioongozwa na Naibu Waziri wa (EAC) wa Tanzania, Bw. Abdallah Sadallah.
Katika Mkutano huo, ambao mtu wa kwanza kuzunguza na wananchi katike eneo hilo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa Kagera, Kanali Fabian Massawe ambaye katika utambulisho wake alilazimika kujibu mapigo kwa kutumia lugha ya Kiswahili bila kuchang’anya na lugha ya kiingereza katika mkutano wake wote.
Akizungumza katika mkutano huo, Kanali Massawe alisema lugha ni kitu muhimu na ili waweze kushirikiana ni lazima itafutwe lugha moja itakayotumiwa katika mawasiliano na kuelewana tofauti na hivi sasa, ambapo kunajitokeza mkanganyiko.
“Lugha ni kitu muhimu na ya msingi sana katika mawasiliano, na ili tuweze tushirikiane, itafutwe lugha moja ya mawasiliano hata kama ni Acholi, Kiganda, kihaya …..lakini mambo ya kutumia makalimani ni kuonesha udhaifu wa ushirikiano wetu”alisema.
Alisema iwapo itapatikana lugha yoyote moja itakayokubalika kutumika jumuiya hiyo wananchi pamoja na viongozi wao hawana budi kukijifunza kwa bidii, kwa ajili ya maendeleo yao.
“Hebu angalieni Wazungu mfano kama Marekani wanatumia lugha gani kuu ya mawasiliano… wao wamechagua lugha moja ya mawasiliano na ndiyo maana wameweza kupiga hatua”aliongeza.
Hata hivyo, aliwaomba viongozi wanchi hizo kutumia vyombo vya habari vya kijamii vilivyoko mikoani katika kuelimisha wanachi juu ya shirikisho hilo kwani vyombo hivyo navyo vina nguvu katika jamii inayowazunguka.
Naye Naibu Waziri Mkuu wa nchini humo, Bw. Kategaya akizungumzia historia ya Kiswahili nchini Uganda alisema wananchi wengi wao wanajua kuwa Kiswahili ni lugha ya majambazi wanaopora mali za wananchi na askari wanaoitumia kwa kutoa amri hali iliowajengea woga wananchi na kukichukia.
Alisema licha ya lugha ya Kiswahili kuchukuliwa kwa mtizamo huo, lakini katika kiserikali ni lugha ya mawasiliano na ni lugha kuu inayotumiwa na watu wengi wa Afrika Mashariki.
Alisema pamoja na hali hiyo, kupitia wizara yake na ya elimu nchini humo, unafanya mpango ambapo hadi kufika mwakani lugha hiyo itaanza kufundishwa kuanzia elimu ya msingi lengo likiwa ni kutaka kukiendeleza ili wananchi wa nchini humo waweze kukielewa katika mawasiliano.
Katika kikao kilichofanyika juzi nchini humo katika ukumbi wa Juuko’s wilayani Rakai baadhi ya viongozi wa nchini humo, wakioongozwa na Mkurugenzi (CHO) wa wilaya hiyo,Nkato James walionesha wazi kukibeza lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya saba duniani kwa madai kuwa hawajisikii vizuri kukizungumza, ambapo walitaka lugha ya kiingereza na kiganda ndizo zitumike.

Katika mkutano huo wa siku mbili ulilenga
kujadili masuala ya ushirikiano wa jumuiya ya Afrika Mashariki, mafanikio,
fursa na changamoto zinazozikabili nchi wananchama kati ya Tanzania na Uganda
kwa upande wa maeneo ya mipakani.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment