Thursday, April 26, 2012

Leo ni siku yangu ya kuzaliwa, asante Mungu kwa kunibariki.

Leo ni Aprili 26,2012, ninatimiza MIAKA kadhaa ya kuzaliwa.Namshukuru sana Mungu wangu muumba wa mbingu na nchi na kila kitu kilichomo hapa duniani, kwa kuniwezesha kufika hadi siku hii ya LEO.
Nashindwa hata namna ya kumshukuru Mungu kwani sielewi ni kwa nini bado ananipa pumzi ya kuvuta hewa ya dunia hii.Lakini katika hili najipa moyo na kuamini ni jinsi gani pendo la MUNGU HALICHUJI na  Pendo lake lilivyo la milele, bado ananipenda!, bado ananihitaji nielendelee kuishi katika uso wa dunia hii.
Siku kama hii ya leo, mama yangu aliyenizaa hawezi kusema ni namna gani labda mimba yangu ilivyomsumbua, lakini kwa uwezo wa Mungu nilizaliwa salama salimini.
Oh, Mungu wa Upendo naomba uendelee kunipa baraka zako ziniwezeshe kuendelea kukupenda kwani hapa duniani kumejaa vishawishi vingi, kupitia SHETANI Mwovu anayerandaranda kila kona za nyoyo za Wanadamu ili wamfuate.Lakini naamini kwa jina lako TAKATIFU utaniepusha na vishawishi vya huyo IBILISI.
Mungu niepushe na wale binadamu wenye roho za kishetani, wanaochukia binadamu wenzao bila sababu zozote za msingi, niepushe na binadamu wasio kuwa na moyo wa ustahimilivu, niepushe na wanadamu wasio penda maendeleo na wenzao.Niepushe na binadamu wasengenyao wenzao,waliojaa hila,wasiopenda wenzao wapate.Niepushe ni watu wanaojipenda wenyewe zaidi ya wenzao, wanaojiona wao ndiyo bora kuliko viumbe vyako vingine hapa duniani.
Mungu tujalie uwezo na nguvu za kupendana sisi wanadamu, imarisha upendo kati ya familia yangu, ukoo wafanyakazi wenzagu N.K.
MUNGU ibariki nchi yangu Tanzania, nuru yako iwake na ing'arishe wa wale wote wanaokuchaa.
Aksante Mola kwa kuzidi kunipenda, pendo lako linazidi kunipo faraja ya kuendelea kuishi hapa dunia na kuzidi kukutumikia.AMENA.
 

No comments:

Post a Comment