Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Musoma,Gasper Kasanda Amworo akisoma wasifu wa marehemu Mzee Alloyce Amworo (90) katika Misa Takatifu iliofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Ingri.
Mchungaji Kasanda akiwa sambamba na mke wa marehemu kaka yake Alloyce na shemeji yake marehemu, Bi. Aoko wakiongozana kuingia kanisani katika misa ya kumwombea marehemu.
Fundi akisakafikia kaburi muda mfupi kabla Marehemu Alloyce kupumzishwa humo, hapa ni kijiji kwake Randa, Kata Kigunga Wilayani Rorya
Padri wa Kanisa katoliki Parokia ya Ingri, Romanus Ciupaka akiangaliajeneza lililobeba mwili wa marehemu Mzee Alloyce Amworo (90) ukishushwa ndani ya gari kwa ajili ya kuingizwa kanisani huku akipokea tayari kuupokea na kuuombea tayari kurejeshwa nyumbani kwake kwa ajili ya kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele.
Baadhi ya waombolezaji waliohudhiria katika mazishi ya Mzee Alloyce Amworo kijijini kwake.
Mmiliki wa Blogi hii aliyesimama akibofya simu yake, akiwa msibani hapo.
Sehemu ya wanakwaya wakiimba ndani ya kanisa.
Baadhi ya wajukuu, na wakwe wa marehemu wakiwa katika picha ya pamoja na dada wa marehemu, aliyekaa kwenye kiti akiwa amebeba chupa ya maji mkononi, Bi. Magreth Amworo(97) muda mfupi baada ya kuwasili kutoka nchini Kenya alikoolewa.
Hawa ni baadhi ya ndugu wa mke wa marehemu wakiwa wanamliza wakiwa jijini mwanza kabla ya maiti kusafirishwa kwenda Mara, Rorya.
No comments:
Post a Comment