Mwili wa nguli wa tasnia ya uigizaji hapa nchini, Steven Kanumba (28) the Greater unafanyiwa uchunguzi leo katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili.
Habari zilizozifikia Blog hii leo mchana, mwili huo tayari umeshaanza kufanyiwa uchunguzi na wataalam wa Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ambapo taarifa kamili ya kifo chake itaweza kuanikwa kwa jamii.
Aidha muigizaji binti mdogo na mwenye makeke katika tasnia hiyo ambaye inadaiwa kuwa alikuwa mpenzi wake bado anashikilia na kituo cha polisi mkoa wa Kinondoni kwa ajili ya mahojiano zaidi kutokana na wakati kifo kikimpata Kanumba alikuwa naye chumbani.
Kanumba alifariki dunia usiku wa kuamukia Jumamosi 6 Aprili, mwaka huu saa 9. usiku nyumbani kwake Sinza Vatican Jijini Dar Es Salaam.
Kanumba anatarajiwa kuzikwa Kesho Jumanne, katika makaburi ya Kinondoni, baada ya mama yake kudhiriwa kuzikwa jijini humo badala ya kwao Shinyanga alikozaliwa.
Bwana ametoa, Bwana ametoa jina lake Bwana lihimidiwe.AMEN
No comments:
Post a Comment