Na Theonestina Juma, Bukoba
UGAWAJI na uuzaji wa viwanja 5,000 katika Manispaa ya Bukoba kati ya mwaka 2003 na 2008 hatimaye utekelezaji mkakati wake umeanza kutekelezwa baada ya kutolewa ratiba ya shughuli hiyo.
Kwa mujibu wa Afisa Mipango miji katika Manispaa ya Bukoba, Bw. Catres Rwegasira, utekelezaji wa mkakati wa uuzaji na ugawaji wa viwanja hivyo, umeshaanza ambapo kwa sasa tayari mauzo ya fomu kwa wanaotaka kununua kiwanja umeshaanza kupitia benki ya posta tawi la Bukoba pekee.
Bw. Rwegasira alisema kutokana na suala la ardhi limekuwa moja yasababu inayochangia migogoro wa maendeleo ya mji wa Bukoba mwaka 2008 Manispaa ya Bukoba kupitia Mpango Mkakati kwa ufadhili wa UN-HABITAT ilipima viwanja 5000 katika maeneo mbali mbali ya mji wake ili kuharakisha uwekezaji na kupunguza ujenzi holela.
Alisema kulingana na ugawaji wa viwanja hivyo utazingatia vigezo kadhaa mbazo alizilitaja kuwa ni pamoja na kuwapatia kipaumbele cha kwanza wananchi wote ambao ardhi yao imetwaliwa kwa ajili ya upimaji wa viwanja 5,000.
Pia alisema kipaumbele kingine utazingatia wananchi waliochangia gharama za upimaji wa viwanja 800 tokea mwaka 2003 ambao hadi leo hawajapatiwa kiwanja .
Hata hivyo alisema wenye viwanja vilivyotwaliwa kupisha upimaji wa viwanja 5,000 watakaoomba mita za mraba 400 hadi 800 (High density) watapunguziwa kiasi cha sh. 400,000.
Akizungumzia waliochangia gharama za viwanja mwaka 2003 Bw. Rwegasira alisema wananchi wapatao 621 walithibitisha kutumia risiti za malipo kuwa walichangia gharama za upimaji wa viwanja takribani miaka tisa iliopita, ambapo kiasi kilichochangwa kinatofuatiana kuanzia sh. 10,000 hadi 200,000 ambapo kiasi hicho kilikuwa ni sh. milioni 35,515,000.
Aliasema ili kupata thamani ya gharama ya sasa iliochangwa, fomula ya kibenki imetumika ambapo riba kwa wastani ni asilimia tano kwa benki nyingi kwani ni muda tangu fedha hiyo iwekwe ni miaka tisa hadi sasa.
Alisema kiasi kichochangwa kwa thamani ya sasa ni sh. milini 55,095,421 ili kuweza kufidia wananchi ambao hawakuweza kujiorodhesha kiasi cha sh. milioni 20 kimeongezwa na kufanya gharama ya sasa kuwa sh. milioni 75,097.421 ambapo uchangiaji huu wa gharama za upimaji hauna uhusianao wowote na mradi wa viwanja 5,000.
Alisema kutokana na fedha hizo zilipokelewa na Halmashauri hivyo, Manispaa itawajibika kurejesha fedha hiyo au kuwauzia viwanja kwa utaratibu ambao hautaathiri makubaliano yao walioingia baina ya UTT na Manispaa ya upimaji wa viwanja 5,000 vilivyogharimu kiasi cha sh. bilioni 2.9 kwa makubaliano ya kugawana faida baada ya kuuza viwanja kwa uwiano wa asilimia 60 kwa UTT na asilimia 40 kwa Manispaa ya Bukoba.
Hata hivyo, upimaji wa viwanja hivyo uliofanywa na Chuo cha Ardhi Morogoro, ambapo kazi hiyo imeshakamilika na kati ya viwanja 4923 vilivyopimwa viwanja 2646 sawa na silimia 53 tayari vimeidhinishwa na Mkurugenzi wa upimaji Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi .
Alisema viwanja vingine takribani 2313 bado vipo Wizarani kwa mujibu wa Mkandarasi , ifikapo mei 5 mwaka huu viwanja vyote vitakuwa vimekaidhinishwa na kusajiliwa.
Hata hivyo kwa upande wa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dkt. Anatory Amani alisema kwa historia, Manispaa ya Bukoba itakuwa ya kwanza kupima viwanja na kupitisha barabara kabla ya kuvigawa.
Alisema Mkandarasi wa kutengeneza baadhi ya barabara katika maeneo ya mradi ameshapatikana ambapo kwa sasa kazi ya upasuaji na utengenezaji wa barabara mpya mkubwa na ndogo zimenza kuwekwa ambapo jumla ya kilomita 54.8 zitatengenezwa katika maeneo hayo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment