Hawa ni baadhi ya wajukuu, wakiwa porini wakimburia Mzee Alloyce Amworo (90) wakiwa wamejipumzisha porini wakifunga bendera, pamoja na vitu vingine huku ng'ombe hawako pichani wakielendea kupata majani.Kuburu ni kitendo cha kuswaga ng'ombe wa marehemu pamoja na wana ukoo na kupelekwa kwenye malisho huku wakipiga ngoma na kuimba mbali na mji wa mtu aliyefariki, ambaye mara nyigi huwa ni mwanaume aliyeoa na kuacha mji wake kulingana na mila na desturi za kabila la Waluo, hatua hii inakuwa ya mwisho ikiwa ni siku ya kuanua matanga.Kwa kawaida wajukuu wakiume na na wakike pamoja na wasichana wa ukoo huo walioolewa ndiyo huwajibika kufanya shughuli hiyo, ambapo hulazimika kuondoka msibani asubuhi kuanzia saa 1.Na hutakiwa kurejesha mifugo hao kuanzia saa tisa alasiri na kuelendelea.Ni lazima kuwepo kwa bendera za khanga zinazofungwa na wanawake.
Baadhi ya wajukuu waliokuwa wakikabiliwa na shughuli maalum ya kuburu kwenye msiba wa babu yao wakiwa katika picha ya pamoja na mumili wa Blog hii aliyevaa kitambaa cheusi shingoni.Hapa wakiwa tayari kuelekea msibani wakiwa wamejifunga majani hayo maalum kwa ajili ya shughuli hiyo pamoja na kujipakaa na kujichora mwilini kwa kutumia udongo maalum ambao mara nyingi hupatikana maeneo ya mito.
Hapa baadhi ya wabururaji wakiwa kwenye kaburi la Mzsee wetu wakibaki kushang'aa yanayotokea katika tukio hilo.
No comments:
Post a Comment