Biharamulo
KATIKA hali
isiyo ya kawaida, askari Jeshi (JWTZ) wapatao tisa wanadaiwa kumvamia Katibu
Tawala wa Wilaya ya Biharamulo ofisini
kwake na kuanza kumshushia kipigo kikali hadi kumvunja jino moja taya na
kumjeruhi sehemu mbali bali mwili.
Tukio hilo
la kusitisha katika idara ya utumishi wa umma, lilitokea Aprili 18, mwaka huu
saa 9 alasiri wilayani humo.
Sababu za
kumpekelea Askari Jeshi la wananchi (JWTZ) kumvamia Katibu Tawala wa wilaya
hiyo ofisini kwake , Bw.Msoud Biseyamaga kwa madai ya kukamata pikipiki mmoja inayodaiwa
kumilikiwa na mmoja wa askari jeshi hao wakati zoezi la kufanya usafi wa mazingira
ukifanyika kama ilivyo kawaida.
Akizungumza
na waandishi wa habari wilayani humo, Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Bw. Ernest
Kahindi amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo, ambapo amedai kuwa kitendo cha viongozi hao kupigana tena
ndani ya ofisi ikizingatiwa wote ni wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama wa
wilaya hiyo, ni udhalilishaji na umevunja mpaka wa utumishi.
Alisema
viongozi hao wamedhalilisha na kuvunja utaratibu, kanuni , sheria na maadili za
utumishi wa umma, ambapo uataribu unafanyika wa kukaa kwa kamati ya ulinzi na
usalama wa wilaya ili kuangalia ni hatua gani za kisheria zinaweza kuchukuliwa
dhidi yao.
Mkuu wa
wilaya ambaye wakati wa tukio hilo likitokea hapokuwepo ofisini kwake, ambapo
kwa maelezo yake alisema kuwa alikuwa hospitali ya wilaya alisema kuwa awali
alipata taarifa kuwa katibu Tawala na CO wanapigana ilimlazimu kuja mbio
ambapo walipofika ofisini kwa katibu tawala huyo walimkuta akiwa amejificha
ndani ya mmoja ya chumba ndani ya ofisi yake baada ya kupigwa na Wanajeshi hao.
Hata hivyo,
kwa upande wa Mganga wa hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo,Dkt. Grasmus Sebuyoya
akizungumza na waandishi wa habari hopitalini hapo, alikiri kumpokea Katibu
tawala huyo, ambapo alipopimwa amekutwa akiwa amepasuka taya yake, kungo’olewa
jino moja la juu na kuumizwa jicho lake la kushoto.
Alisema maumivu hayo yanaonesha kuwa alipigwa sehemu
mbali mbali hasa kichwani kwa nguvu.
Hata hivyo,
katika tukio hilo ambalo ni ndara kutokea, chanzo cha ugomvi huo ulitokana na
sheria ndogo ilipo mkoani hapa ya kila wilaya inapaswa kupanga siku yake ya
kufanya usafi, ambapo kwa wilaya ya Biharamulo siku ya kufanya usafi ni kila
jumatano ya kila wiki.
Kutokana na
siku hiyo, hakuna mtu yeyote anayeruhiswa kufanya kazi yoyote hasa za
kibiashara hadi ifikapo saa nne asubuhi.
Hatua ya
kufikia katibu Tawala huyo anadaiwa kukamata pipiki moja ambayo hata namba yake
ya usajili haijajulikana ikiwa inaendeshwa na mtu anasiyemfahamu bila kujua
kuwa ni ya mmoja wa wanajeshi hao wa
wilayani humo.
Hata hivyo,
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Henry Salewi alipoulizwa na blog hii juu
ya tukio hilo alidai kuwa hajapata taarifa zozote juu ya sakata hilo na kwamba
labda blog hii imuulize Mkuu wa wilaya ya Biharamulo au Mkuu wa Mkoa
Kagera, Kanali Fabian Massawe.
mwisho.
No comments:
Post a Comment