Mamia wa waumini wa Kanisa Katoliki kutoka ndani na nje ya nchi, wakiwa katika Parokia ya Mugana ambapo Oktoba 30, kila mwaka hufurika katika eneo hilo kuhiji.Waliovaa mavazi meupe katikati ya umati wa watu, ni Mapadri wa kanisa hilo kutoka ndani na nje ya nchi.
Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, hivi ndivyo hali inavyokuwa Oktoba 30 kila mwaka, katika kituo cha kuhiji cha Mugana Wilayani Missenyi, ambapo idadi ya watu wanaojitokeza hawahesabiki, lakini cha ajabu watu wanaofika katika hili wanakuwa watakatifu kweli, kwani hata vibaka hawaonekani kwani kila mmoja anakuwa na mshike mshike wake wa kutaka kuondoka na maji ya baraka.(Picha zote na Theonestina Juma)
No comments:
Post a Comment