Aliyesimama upande wa kushoto ni mumiliki wa blog hii (Theonestina Juma)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya ndugu zake, ambao ni Happiness Odira, aliyevaa fulana ya njano na anayemfuatia ni Euphrasia Juma, tukiwa tayari kushiriki kikamilifu katika mambo fulani za kimila huko kijijini kwetu, Rorya Mara.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali Fabian Massawe aliyesimama nyuma ya baadhi ya wanahabari ofisini kwake akiwa amebeba mkononi kinasa sauti kwa lengo la kuwawezesha waandishi wa habari kusikiliza wimbo maalum aliourekedi, uliotungwa na kuimbwa na bandi la Kakau (Kanisa Katoliki na Ukimwi) mjini Bukoba kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo ya Mkoa wa Kagera.
Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Henry Salewi akiangalia kwa makini pombe iliotengenezwa kwa ndizi maarufu kama 'banana Wine' katika maonesho ya siku ya mkulima wa migomba Mkoa wa Kagera.Kinywaji hiki kinadaiwa kuwa na kilevi asilimia saba.
Profesa Swenner Rony huyo mzungu aliyesimama na kuvaa shati nyeupe, kutoka chuo kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji aliyesaidia kuboresha mradi kiutaalam na ushauri katika kuendeleza zao la Migomba mkoani Kagera akiwa anakula balagara iliotengezwa kwa ndizi, hapa alikuwa katika maonesho ya siku ya zao la migomba mkoa Kagera yaliofanyika wilayani Ngara.
No comments:
Post a Comment