Ndizi aina ya gonja iyoliwa ikiwa imechomwa kwenye moto au mafuta ya kupikia.
Mkulima wa migomba aina ya FHIA wa kijiji cha Kasulo Wilayani Ngaram, Bw. Samuel Kaparala akiwa katika maadhimisho ya siku ya migomba Mkoa Kagera.
Pori la Kimisi iliokuwa ikitumiwa na majambazi kujificha wakati wakiteka magari ya abiria, pori hili kwa sasa magari yanapita bila kusindikizwa na askari polisi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kabla ya ujio wa Kamanda Tossi.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Fabian Massawe mwenye tai jekundu akisiliza maelezo kutoka kwa Mratibu wa zao la Migomba Taifa, Bw. Mugenzi Byabachwezi namna ya kutunza zao la migomba wa pili upande wa mkono wa kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Kanali Salum Nyakonji.
Taswira katika Taifa, hawa ni baadhi ya watoto wa kijiji cha Rusumo waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya mgomba Kagera yaliofanyika hapo kijijini kwao.
Kikundi cha Mshikamano kinachojishughulisha na kilimo cha migomba ya kisasa wakicheza ngoma katika maadhimisho ya siku yao.Tangu miaka 750 iliopita hakujawahi kuwepo maadhimisho ya siku ya migomba nchini, wala duniani.Haya ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya migomba kufanyika hapa nchini, ndani ya mkoa wa Kagera Wilayani Ngara.
No comments:
Post a Comment