Monday, April 30, 2012

'Hatuondoki, hata kama mkiwaleta kikosi cha FFU'-Wafanyabiashara Soko Kuu Bukoba

UJENZI wa soko kuu la kisasa katika Manispaa ya Bukoba huenda' ukaingiwa na mchanga' kutokana na wafanyabiashara wote wa  soko hilo kusema kuwa hawako tayari kuondoka humo kupisha ujenzi huo.
Wafanyabiashara hao walifikia uamuzi huo juzi katika mkutano wao wauliofanyika ndani ya soko hilo kujadili hatma yao baada ya kuondoka ndani ya soko hilo kupisha ujenzi kuanza.
Wafanyabiashara hao waliokuwa wakizungumza kwa jazba walidai kuwa hawajashirikishwa kikamilifu na ujongozi wa Manispaa ya Bukoba juu ya ujenzi wa soko hilo la kisasa tangu mwanzo ambapo kwa sasa ndiyo wanashang'aa wakielezwa kutakiwa kuondoka sokoni hapo kupisha ujenzi wake ambao utagharamu kiasi cha sh. bilioni 11.
Hao wanaotuambia kuwa tuondoke ndani ya soko, twende wapi... wakati sisi baadhi yetu wamekopa fedha katika taasisi mbali mbali za fedha kama FINCA, CRADB, sasa tutatoa wapi fedha za kurejesha? Tunawatoto watutegemea, kila kitu ndani kinaangalia hii kazi yetu tutaenda wapi? alisikika mmoja wa wafanyabiashara ndani ya soko hilo alihoji.
Wafanyabiashara hao walidai kuwa wanashangazwa kuona miradi mitatu mikubwa yanatekelezwa kwa mkupuo ndani ya Manispaa ya Bukoba, bila mpangilio unaoeleweka kwa wananchi ambapo kwa mawazo yao walishauri kuwa itekelezwe mradi moja baada ya nyingine.
Walisema wao wanashang'aa kumsikia Mstahiki Meya  wa Manispaa ya Bukoba, Dkt. Anatory Amani akizungumza kupitia redioni kuhusiana na ujenzi wa soko hilo na kutakiwa wao wafanyabiashara kuondoka kupisha ujenzi huo bila kwenda kwao kuzungumza nao.
Miradi mkubwa inayotarajiwa kuanza kutekelezwa na Manispaa ya Bukoba ni pamoja na ujenzi wa jengo la kitega uchumi ghorofa 10, itakayogharimu kiasi cha sh. bilioni 20, ujenzi wa kituo cha mabasi sh. bilioni 1 na  ujenzi wa barabara za lami sh. bilioni 6.
Katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Bukoba kilichofanyikaAprili 16 mwaka huu, kiliafikia kuanza kwa ujenzi wa soko hilo, ili kuwezesha mji wa Bukoba kuweza kuonekana tofauti na miaka mingine kutokana na kuwa kongwe lakini maendeleo ikiwa ni ZERO.
Hata hivyo, katika uchunguzi wa blog hii umebaini kuwepo kwa kundi la watu wasioitakia maendeleo Manispaa ya Bukoba, ambapo tatizo lingine likiwa ni baadhi ya viongozi walioko madarakani pamoja na baadhi ya wanasiasa kupingana wenyewe kwa wenyewe kwa ubinafsi tu.
Katika kikao cha Baraza la Madiwani, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Bw. Robert Kwela, aliwaambia Madiwani hao kuwa tayari yameshafanyika mazungumzo zaidi ya mara mbili kati ya uongozi wa Manispaa na wafanyabiashara hao, namna watakavyoweza kupisha ujenzi huo kwa kutawanyika katika baadhi ya masoko yalioko mjini hapa.
mwisho.


No comments:

Post a Comment