Monday, April 30, 2012

Kwa wenzetu wa nchi jirani ya Uganda usalama uko hivi

Ndugu yangu eh kuingia humu ni kwa kufuata mstari maalum usidhani uko TZ, hawa ni baadhi ya wananchi waliokuwa wakihudhuria katika mkutano wa kujadili  Shirikisho laJumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kati ya Tanzania na Uganda wakikaguliwa kwa kifaa maalum, kabla ya kuingia uwanja wa mpira wa Malaba wilayani Rakai Nchini Uganda, anayekaguliwa  na polisi huyo wa Uganda ni Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Mkoani Kagera, Bw. Phinias Bashaya.
 Wee..panga mstari Bwana, mbona kana kwamba uko nje ya mstari ndivyo inavyoonekana huyu askari wa nchini Uganda akimwambia mtu anayetazamana naye.
 Haya , ukaguzi kwa kutumia kifaa maalum ukiwa umepamba moto kwa wageni waalikwa wa mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa pande zote mbili Uganda na Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja, wa tano kutoka upande wa kushoto ni Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa EAC nchini Uganda, Bw. Eriya Kategaya, wa kwanza upande wa kushoto ni Mkuu wa Mkoa Kagera Kanali Fabian Massawe, wa kwanza upande wa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, anayemfuatia ni Naibu Waziri wa EAC Tanzania, Dkt. Abdallah Sadallah na anayemfuatia wa tatu kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Missenyi, Kanali Issa Njiku.
Jamani bado mnaendelea kuchukua sura zetu, mmmh hawa ni viongozi hao katika picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment