Na Theonestina Juma, Bukoba
HALMASHAURI ya Manispaa ya Bukoba, Mkoani Kagera inatarajia kujenga soko kuu la kisasa utakaogharimu kiasi cha sh. bilioni 11.
Hayo yamesemwa jana jioni na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dkt. Anatory Amani katika kikao maalum cha baraza la Madiwani kilichoitishwa kwa lengo la kuidhinisha malipo ya Mhandisi Mshauri ya sh. milioni 500 na mikopo ya sh. milioni 200.
Mstahiki meya huyo alisema lengo la kujenga soko kuu hilo la kisasa ni kutokana na kutaka mabadiliko katika Manispaa ya Bukoba, ambayo miaka nenda rudi haibadiliki.
Alisema Manispaa ya Bukoba wanatarajia kukopeshwa sh. milioni 200 na Benki ya uwekezaji (TIB) kwa sharti la kurejesha fedha hizo, kwanzia sasa hadi Oktoba 30 mwaka huu na riba ya asilimia nane ambazo ndizo atapewa Mhandisi Mshauri, ambapo pia TIB itawapa Manispaa hiyo msaada wa sh. milioni 90
Malipo ya milioni 300 zinazobaki yatalipwa Mhadisi Mshauri katika mwaka wa fedha ujao 2013/2014 ambapo ujenzi huo unatarajia kuchukua miaka mitatu kulingana na maelekezo ya Mhandisi Mshauri atakayotoa baada ya kuanza utekelezaji wake.
Hata hivyo, kabla ya kufikia muafaka huo, baadhi ya madiwani walionekana kupingana na uongozi wa Manispaa hiyo kwa madai kuwa hawawezi kupelekeshwa kama watoto katika kusaini mktaba mkubwa hivyo ambayo inaweza kuwatia hasara wananchi wao.
Aidha baadhi ya madiwani hao, walisema uongozi wa Manispaa hiyo ulikiuka sheria za uendeshaji wa baraza hilo mojawapo likiwemo kutoaalikwa kwa njia ya barua ambapo baadhi yao walidai kualikwa kwa kupiga simu kuja kupitisha mkataka mkubwa kama huo.
“Siwezi kuendeshwa kama mtoto, mimi sio mtoto, tunaitwa kuja kuridhia mkataba mkubwa kama huu wa ujenzi wa soko… bila kupewa ripoti, hata ajenda za kikao hakuna…hata huo mkataka tunaotaka kuridhia hatujauona kwa maandishi…siko tayari kupitisha mkataba huu”alisema Diwani wa Kata ya Kitendaguro ambaye pia aliwashi kuwa Mkuu wa Mkoa Kagera wa wakwanza na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba aliyemaliza muda wake mwaka 2010, Bw. Samuel Ruangisa.
Alisema mkopo wa sh. milioni 200 ni ‘commitment’ kubwa ambayo haina haraka kwa sababu ni fedha za wananchi.
Bw. Ruagisa alisema kama mkataba huo ukiridhiwa na baraza hilo atatoka kikaoni ambapo alitekeleza hivyo, kwani madiwani hao kuridhia ujenzi huo kwa kishindo, Bw. Ruangisa alikusanya kila kilicho chake na kuondoka ukumbini 12.10 jioni hakurudi tena mpaka kikao kiahairishwa.
Hata hivyo, kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Bw. Robert Kwela tatizo kubwa lililojitokeza ni kwamba Bw. Ruangisa hakuwepo muda mrefu hapa mjini na vitu vingi vimempita na kwamba kuhusu mialiko madiwani wote walialikwa kwa njia ya maandishi.
Hata hivyo, kwa upande wa Mstahiki Meya Dkt. Amani alisema mtakaba wa ujenzi huo yuko tayari kumpatia mheshimiwa yeyote kusoma na kwamba diwani yeyote yuko huru kwenda kwa Mkurugenzi kuomba nyaraka aina yoyote na kusoma.
Alisema katika mkataba huo Mkurugenzi tayari ameshapitia vipengere vyote muhimu hasa vinavyohusiana na sheria na kwamba kwa sasa anashangaa kuona mambo mengine yakijitokeza.
Hata hivyo, ujenzi hio ambao uliridhiwa na takaribani madiwani wote, wakichangia hoja hiyo, baadhi ya madiwani waliupongeza uongozi wa Manispaa hiyo kwa ubunifu wao wa kutaka kuleta mabadiliko ndani ya Manispaa ya Bukoba.
Diwani wa kata ya Miembeni, Bw. Richard Gasper (CCM) alisema kwa miaka nenda rudi Manispaa ya Bukoba hakuna hata mradi wwote mkubwa ambao umeshawahi kutekeleza, na hivyo kwa sasa hawatakiwi kurudi nyuma kama mipango yote yameshakuwa tayari.
“Mstahiki Meya unajua mtu akisikia sh. bilioni 11 kwanza anawazia hamna chake pale?.... pamoja na sisis kujulikana kama ‘Nshomile’ wasomi lakini hawana taha nyumba ya ghorofa ambayo mgeni akifika anashangae, watu wamebaki kutubeza tutabezwa mpaka lini katika suala nzima ya maendeleo?alihoji.
“Tusiogope kukopa, bila mikopo hakuna maendeleo, bila mikopo hatuwezi kwenda mbele, mimi hapa nimeweza kupata maendeleo kutokana na mikopo kwa sasa nadaiwa zaidi ya milioni 30 za mikopo”alisema Diwani Gasper huku akipigiwa makofi na Madiwani wenzake.
Naye Diwani wa Kata ya Bakoba, Bw. Felician Bigambo (CUF) alisema uongozi wa Manispaa ya Bukoba wakiongozwa na Meya wao hawapaswi kukata tamaa pale wanapoona shida wakae chini kujadiliana lengo walete mabadiliko ndani ya Mnaispaa ya Bukoba licha ya kuwa watakutana na vikwazo vingi.
Hadi sasa kumeshafanyika vikao mara mbili kati ya wafanyabishara wa soko kuu mjini hapa na uongozi wa Manispaa juu ya mstakabali wao wakati soko hilo litavunjwa na kuanza kujengwa upya, juu ya wapi waelekee kutokana na baadhi yao wanamikopo na wanatakiwa kurejesha, na kivipi watatunza mali zao kwa kipindi hicho.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment