Tuesday, July 3, 2012

Wananchi walala porini, kukwepa kamatakamata ya polisi-Kisa mgogoro wa ardhi wanamlinda kigogo

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kyaya wakizungumza na wanahabari juu ya askari polisi kuwavamia kwenye nyumba zao usiku wa manane na kuwakamata wenzao watano akiwemo mtoto wa mwaka mmoja na nusu na kuswekwa rumande.
Kijana huyu ambaye ni mkazi wa mtaa wa Kyaya akiwaonesha wanahabari dirisha la Nyumba ya Bw. Richard Ifunya (60) lililobomolewa na askari polisi waliowavamia nyumba tano za wakazi wa mtaa huo
Wananchi wa mtaa huo wa Kyaya wakiwaonesha waandishi wa habari nyumba ya Bw. Robert (27) alivyovunjiwa mlango la askari hao.
Jamani huu mlango haungi, umeegeshwa tu ndivyo polisi walivyoamua kumfanyia unyama mumiliki wa nyumba hii.



Hii nyumba kutokana na uimara wake kuanzia ukuta na mlango wake, polisi walilazimika kugonga juu ya mlango huo kwa lengo la kutaka kubomoa ili kuingia ndani kumwondoa mwananchi asiyekuwa na silaha wala asiyetuhumiwa kumuua mtu.Nyumba hii pia kufuli uliwekwa tu ilmradi lakini polisi walifanikiwa kuuharibu kama walivyodhamiria.

Hapa wanahabari hao walilazimika kutembea nyum,ba moja baada ya nyingine lengo kuangalia ni namna gani haki za binadamu zinazvyokiukwa na Jeshi la polisi kwa kipindi hiki wakihubiri polisi jamii kila kona, wakati wakiwa wao ndiyo wa kwanza kuvunja huo mfumo wa polisi jamii yao.




No comments:

Post a Comment