Na Theonestina Juma,
Bukoba
KAMPUNI ya bia ya safari Lager imetoa vifaa vya michezo kwa timu saba za mchezo wa pool zinazotarajia kuanza kuchuana leo (kesho) ambapo bingwa anatarajiwa kuzawadia sh. 700,000 taslim
Vifaa hivyo ambavyo ni fulana , kofia na fedha vimekabidhiwa leo kwa Manahodha wa timu saba za Manispaa ya Bukoba kutoka kwa Msimamizi wa timu ya safari Integrated Communications Ltd, Bw. James Magori ambavyo vilikabidhiwa na Mgeni rasmi, ambaye ni Diwani wa kata ya Bilele, Bw. Ibrahim Mabruk kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dkt. Anatory Amani kwenye hafla fupi iliofanyika katika baa ya Q mjini hapa.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza leo (kesho) Julai 5 hadi Julai 8 mwaka huu ambapo timu itakayoibuka bingwa kwa upande wa mkoa Kagera itajinyakulia kitita cha sh. 700,000 huku mchezaji mmoja mmoja akiondoka na sh. 350,000 kwa upande wa wanaume na wanawake wa kwanza atazawadiwa sh. 250,000 taslimu.
Kwa mujibu wa maelezo ya Msimamizi wa timu ya safari Integrated Communications Ltd, Bw.Magori mshindi wa pili kwa upande wa timu, atazawadiwa sh. 350,000, mshindi wa tatu, 200,000, wa nne sh. 100,000 na kifuta machozi cha sh. 50,000 kitatolewa kwa timu zitakazoshiriki. Copon
Halikadhalika kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja kwa upande wa wanaume mshindi wa pili atapata sh. 200,000, wa tatu sh. 150,000 na wa nne sh. 100,000 ambapo wanaume kwa wanawake wanne kati ya wanane watakaopoteza mchezo katika awamu ya pili watazawadiwa sh. 50,000, na wakataopoteza katika awamu ya kwanza wanane kati ya 16 wataambulia sh. 20,000.
Aidha kwa upande wa wanawake kwa mchezaji mmoja mmoja mshindi wa pili atazawadiwa sh. 150,000, wa tatu sh. 100,000 na wa nne ataambulia sh. 50,000.
Timu zinazoshiriki katika mashindano hayo ya mchezo wa pool katika mkoa wa Kagera ni pamoja na Bukoba, Q bar, Mnyonge, Bilele, Q bar Veteran, Quality na Hamugembe.
Awali mgeni rasmi katika hafla hiyo, Bw. Mabruk aliwataka waamuzi watakaochezesha mchezo huo kuwa waaminifu, waadilifu, watiifu ili mchezo huo uweze kufanyika kwa amani bila kuwepo kwa malalamiko yoyote.
Diwani wa kata ya Bilele ambaye, Bw. Ibrahim Mabruk ambaye alikuwa mgeni rasmi akimkabidhi fedha nahodha wa timu ya Hamugembe Bw. Kelvin Walesi kwa niaba ya timu yake kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo.
“Mimi rai yangu kwa waamuzi wa mashindano haya, tafadhali nawaomba wawe waamini na waadilifu, ili kuwezesha mshindi apatikane kwa haki na amani”alisema Bw. Mabruk.
Katika mashindano hayo ya Bingwa wa taifa wa mchezo wa pool (National Pool Champion) kwa upande wa mkoa wa kagera unatarajia kushirikisha jumla ya wachezaji 53 wanawake wakiwa watano na wanaume 48, mshindi wa kwanza atashiriki katika fainali ya mchezo huo unatarajia kufanyika Jijini Mwanza baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo bingwa wa taifa atalambishwa milioni 5
. Kwa upande wa timu na mchezaji mmoja mmoja kwa wanaume atapata sh. 500,000 na wanawake atavuta sh.350,000.
Hata hivyo, akizungumza na gazeti hili, liliotaka kujua ni kwa nini washiriki wa mchezo huo wote ni wa kutoka katika Manispaa ya Bukoba na si wilaya zote saba za mkoa huo, Mwenyekiti wa chama cha Pool mkoani hapa, Bw. Lyakurwa alisema tatizo ni kutokana na vilabu vingi vya mkoani hapa vinatumia ya mchezo huo ambao hautumii.
Alisema wao wanatumia sheria ya Black ball (Mpira mweusi) ambayo ni ya kimataifa ambapo kwa vilabu vingine vinatumia sheria ya mipira tisa (Nine ball) ambayo ni ya Kimarekani ambapo kabla ya kuanza kwa mchezo huo mwaka jana walijaribu kuzunguka wilaya zote kuwahamasisha kuanza kutumia sheria yao, lakini vilabu hivyo vinaonekana kutokuwa na utayari.
Mwisho
No comments:
Post a Comment