SERIKALI kwa
kushirikiana na kamati ya ulithi wa Dunia ya UNESCO imekubali ombi la
kurekebisha mpaka wa pori la akiba la Selous ili kuruhusu uchimbaji wa madini ya
Urani.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam Waziri wa
Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki alisema kamati hiyo katika kikao
chake cha 36 kilichofanyika juni 24 mwaka huu Saint Petersburg nchini Russia
imekubali ombi hilo.
Kagasheki
alisema tayari kamati hiyo imetenga eneo la Km 200
kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo ambayo yataanzwaa kuchimbwa wakati wowote
kuanzia sasa.
“Mimi
nimerudi kutoka Russia ambapo nilikwenda kuhudhuria mkutano huo kwa niaba ya
serikali, na kwa mara ya kwanza ombi hilo lilipelekwa kwa kamati hiyo ya urithi
wa Dunia ya UNESCO mwezi julai 2011 ambapo lilijadiliwa katika kikao chake cha
35 na hatimaye limekubaliwa mwaka huu” alisema Kagasheki.
Alisema
uamuzi huo ulifanyika ili kuruhusu tathimini ya ardhi mazingira na kukamilisha
kwa kutoa muda kwa wataalamu kufika eneo linarohusika ili kuhakiki taarifa ya
tathimini hiyo.
Wakati
huohuo Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wan chi za Kusini mwa Afrika
utakaofanyika octoba 15 hadi 19 jijini Arusha mwaka huu ukiwa na lengo la
kujadili masuala mbalimbali ya utalii pamoja na uhifadhi katika hifadhi .
Aidha
utajadili changamoto pamoja na mafanikio mbalimbali yakiwemo masuala ya ulinzi
na usalama wa watalii na tanzania imechaguliwa kutokana na usalama wan chi
ulioko hivi sasa na wageni wapatao 300 wanategemea kuhudhuria mkutano huo.
No comments:
Post a Comment