Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Mheshimiwa Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe afungua rasmi mafuzo ya wakufunzi
wa sensa mkoani Kagera jana tarehe 17/07/2012 na kuwaasa wajumbe wa mafunzo
hayo kuzingatia yote watakayofunzwa ili takwimu sahihi za sensa na makazi
ziweze kupatikana kwa ajili ya maendweleo
ya mkoa wa Kagera.
Mratibu
wa sensa mkoa wa Kagera akimkaribisha Mkuu wa Mkoa katika ufunguzinduzi huo
uliofanyika kwenye ukumbi wa Linas Night Club, alisema dhumuni kubwa la mafunzo
hayo ni kuwafundisha wajumbe hao kutoka
katika wilaya zote za mkoa wa Kagera ili watakapoiva wawe wakufunzi wa makarani wa sensa kuanzia ngazi ya Tarafa.
Mkuu
wa Mkoa katika hotuba yake aliwasistiza sana wajumbe wote ambao walitoka katika
kila wilaya kuzingatia sana mafunzo hayo kwa kuhakikisha kila kitu watakachofunzwa
wanakizingatia kwa umakini mkubwa ili kuwa na uelewa mkubwa wa kwenda kuwafundisha makarani kule kwenye tarafa.
Pia
Mkuu wa Mkoa aliwaonya wakufunzi hao kutojihusisha na vitendo vya kubuni au
kukadilia takwimu pale watakapokuwa wanakusanya takwimu kwani ni muhimu sana
kupata tawimu sahihi zitakazosaidia
katika kupanga maendeleo ya taifa zima kwa miaka kumi ijayo. Vile vile
alisistiza sana kuwa taarifa zote za sensa ni siri na hakutakuwa na mtu ambaye
atatoa taarifa za kaya au za mtu binafsi zitakazoulizwa wakati wa sensa.
Wito;
Mkuu wa Mkoa pia alitoa wito kwa
wananchi wote kujitokeza kuhesabiwa siku ya kuamkia tarehe 26/07/2012 kwa kila
sehemu ya mwananchi atayokuwa amelala. Pia alitoa wito kwa Taasisi za dini, na
Taaasisi mbalimbali zote mkoani Kagera
kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kujitokeza na kuhesabiwa. Mhe.
Massawe alitoa angalizo kuwa serikali haitamvumilia mtu yeyote atakaye jaribu kuvuruga
zoezi la sensa, hatua za kisheria zitachukuliwa mara moja.
Mafunzo
hayo ya sensa Mkoani Kagera yanaendeshwa na wakufunzi kutoka ngazi ya Kitaifa,
aidha mafunzo yanayotolewa ni juu ya kutambua maeneo ya sensa, namna ya kuuliza
maswali, namna ya kujaza madodoso pia
mafunzo hayo yanafanyika kwa nadharia na vitendo na mwisho wa mafunzo hayo
wakufunzi watafanya mtihani wa kujaribiwa kuona kama wameiva.
Imetolewa na:
Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa,
Kagera
No comments:
Post a Comment