PICHANI:- Dkt.Askofu Kilaini akimpaka mafuta mmoja watoto kati ya 804waliopata kipaimara leo katika Kanisa la Rumuli mjini Bukoba.
Na
Theonestina Juma, Bukoba
ASKOFU Mkuu Msaidizi
wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Dkt.Methodius Kilaini amewataka wazazi
nchini kuwafundisha watoto kufanya kazi kwa kujituma hata kama wanazo
fedha nyingi kiasi gani za kuwaletea wafanyakazi wa ndani.
Askofu Kilaini
ametoa rai hiyo jana (leo) wakati
akihubiri katika misa takatifu ya kanisa Katoliki la Rumuli mjini hapa ambapo
pia alitoa kipaimara kwa watoto 804 wa
kanisa hilo kutoka katika kata takribani 10 za Manispaa ya Bukoba.
“Wazazi
mnapaswa kuwasaidia watoto wenu kukua kupenda kazi na si kuwa wavivu , msikuze
watoto wenu katika uvivu, wataendelea nao hadi ukubwani ambapo wataanza
kulalamikia maisha magumu, maisha hayawezi kuwa mepesi kama mtu ni mvivu, hata
kama mnazo pesa kiasi gani ya kuwaletea mfanyakazi wa ndani si kila kitu
afanyiwe mwanao, unadhani umanjenga katika mazingira ya aina gani?alihoji.
“Kuna wazazi
wengine wanafedha zao, hawataki watoto wao wateseke,… wanaletea mfanyakazi wa
ndani, ambapo kila kitu anafanyiwa, iwe nguo, kuoshewa vyombo alivyolia … hapa
mzazi hujengi mwanao katika mazingira ya kupenda kufanya kazi bali ya
uvivu, mtoto atakuwa mvivu wa kupindukia akiwa mkubwa….”alisema
Alisema
asilimia kuba ya wazazi ambao waliteseka wakati wa makuzi yao ndiyo huongoza kuwadekeza
watoto wao, ambapo hawataji wanao watekeseke kama alivyoteseka jambo alilosema
kuwa ni kumharibu mtoto zaidi.
Alisema
watoto wanapaswa kukua katika juhudi na si katika uvivu na hilo ni jukumu la wazazi kwa sababu watoto
hao waliopewa kipaimara huu ndiyo wakati wao wa kujenga ama kubomoa.
Aidha Dkt.
Kilaini aliwataka watoto hao wasiwe na akili mgando kutokana na kila mtu
amepewa talanta yake na Mungu na hivyo wanapaswa kuvitumia ipasavyo.
mwisho
No comments:
Post a Comment