Na Theonestina Juma, Bukoba
MWANAFUNZI mmoja aliyekuwa akisoma kidato cha sita nchini
Uganda amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kamba kwa madai kuwa amechoshwa na
wazazi wake kufuatilia maisha yake.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na kamanda wa polisi
Mkoani Kagera, Phillip Kalangi limetokea juzi katika mtaa wa Kashenye katika
Manispaa ya Bukoba.
Mwanafunzi huyo aliyeamua kukatisha maisha yake kwa kujinyonga
ametajwa kuwa ni Remmy Mulima (17) mkazi wa mjini hapa.
Imeelezwa kuwa hadi kufikia hatua ya mwanafunzi huyo
kuchukua jukumu la kujitia kitanzi, ni
baada ya baba mzazi yake ,Bw. Sosithenes
Mulima kumpatia sh. 500,000 kwa ajili ya
ada ya shule, lakini hakuweza kwenda shule na badala yake aliamua
kumchukua hawara yake na kwenda naye
Bunazi wilayani Missenyi.
Alisema wakiwa Bunazi msichana huyo alilazimika kupanga
chumba maalum kwa ajili ya kufanya starehe na hawara yake ambaye hakutajwa jina lake, ambapo baba yake aliweza kupata taarifa hizo
na kwenda Bunazi kumfualia.
Hata hivyo, kutokana na kujua kuwa amefanya kosa, mwanafunzi
huyo alitaka kunywa sumu jambo ambalo baba yake alibaini na hivyo kumzuia.
Mwanafunzi huyo hakuweza kukata tamaa kwani waliporejea
nyumbani kwao mjini hapa ndipo aliweza kuchukua jukumu la kuchukua kamba na
kutundika juu ya miti wa mwembe na kisha kujinyonga huku akiacha ujumbe kwenye nguo
yake kuwa amechoshwa na wazazi wake
kufutilia mambo yake.
Saa ingine njia pekee ni kitanzi shingoni, althought that wa drastic! Angeweza kumwambia mzazi kuwa amechoka na masomo, labda ataendelea baadaye.
ReplyDelete