Sunday, July 8, 2012

Tangazeni injili kwa kuvaa rozari-Askofu Kilaini

Bukoba
RAI imetolewa kwa watoto 804 waliopata kipaimara leo katika kanisa katoliki kuwa watu wa sala hata kama wakichukizwa na jambo kwa kiasi gani.
Aidha watoto hao wameaswa kueneza injili ya kristo kwa kuvaa rozari na si kuivua pindi wakiwa kwenye kundi la watu.
Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu Msaidizi wa kanisa katoliki Jimbo la Bukoba, Dkt. Methodius Kilaini wakati akitoa daraja la kipaimara kwa watopto 804 kutoka takribani kata 10 za Manispaa ya Bukoba katika misa takatifu iliofanyika Rumuli mjini hapa.
 Dkt. Kilaini alisema wazazi wanapaswa kuwahimiza watoto wao kusali muda wote, ili kujikabidhi mikononi mwa Mungu.
"Wahimizeni watoto wanu kusali muda wote, wakitaka kulala usiku, wamkapo asubuhi, wakitaka kula, baada ya kula, wakitaka kufanya jambo lolote hata kujisomea wamkumbuke Mungu kwanza lengo ni kujikabidhi mkononi mwake"alisema Dkt. Kilaini.
Alisema wapo baadhi ya waumini wa kanisa Katoliki ambao wakiwa kwenye kusanyiko la watu wengi huvua rozani waliovaa jambo ambalo linaonesha namna wanavyoshindwa kumtangaza Kristo.

No comments:

Post a Comment