Thursday, July 5, 2012

Wabambwa na dola bandia 102,750/=

JUMLA ya Dola  102,750 za bandia zenye thamani ya sh. bilioni 200 za kitanzania kama zingekuwa halali zimekamatwa na jeshi la polisi Mkoani hapa zikiwa katika harakati za kutaka kuingizwa kwenye mzunguko wa fedha mkoani hapa.

Kiasi hicho  kikubwa cha dola zimekamatwa leo na Jeshi la polisi katika nyumba ya kulala wageni ya Kanoni ilioko mjini hapa, baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema juu ya kuwepo kwa watu watatu waliofika hotelini hapo wakiwashuku kuhusika kuwa na fedha bandia.

Watu wanaoshikiliwa na Jeshi hilo kupatikana na dola bandia hizo ni pamoja na Bw. Boniface Wambura, Bw.Petro Nyakai wote wakazi wa Jijini Mwanza na  Bw. Jimmy Gombo(28) raia wa nchini Kongo ambaye ni mfanyabiashara wa nchini Uganda.
Watu hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani , mara baada ya uchunguzi wa polisi kukamilika.

No comments:

Post a Comment