Friday, July 6, 2012

Maonesho ya saba saba Bukoba hadi mitumba

 Hapa ni maonesho ya saba saba ambapo hadi nguo za mitumba zikiwa zinaoneshwa, Huyu dada aliyenaswa na kamera ya Rorya Kwetu  akisalagua mitumba ambayo ni nguo za ndani zikiwemo sindiria.....,Sabasaba ya Bukoba imejaa bidhaa kutoka Uganda  ambapo bidhaa kutoka Tazania zinazouzwa humo ni chakula, chips kuku na nyama.
 Karibuni kibandani jamani mchague mitumba saaafi, ndiyo maonesho ya saba saba Bukoba.
 Hili ni jengo lililokuwa likijengwa na CCM, limetelekezwa kwa sasa linatumika kwa ajili ya maonesho ya saba saba kila mwaka.Hili eneo kiujumla halitoshi, lakini waandaji walazimisha iwe hivyo hivyo, ilmradi ....
Pamoja na ufunyu wa eneo waandaji wamelazimisha kuwawekea watoto bembea kwani kulingana na vitu vinavyopatikana humo, kama pombe kwa uwingi, watoto wakiingia humo huonekana kuboreka kutokana na kutokuwepo vitu kama hivi.Hapa mwanao ukitaka abembee lazima ulipe sh. 300 hadi 500 kwa muda maalum si kubembea mapaka.

No comments:

Post a Comment