RAI imetolewa kwa waislam wote mkoani Kagera kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchini Agosti 26, mwaka huu.
Rai hiyo imetolewa jana na Sheikh Mkuu wa Mkoani Kagera, Haruna Kichwabuta katika taarifa yake kwa vyombo vya habari mkoani hapa.
Alisema sensa ya watu na makazi ni muhimu katika ustawi wa nchi kutokana na kuisadia serikali kuandaa mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.
Sheikh Kichwabuta alisema kwa maelezo hayo pia ambayo yametolewa nakiongozi wao Mkuu Muft Shehe Shabaan Bin Simba wanahimiza waislam mkoani hapa kuzingatia hayo.
Halikadhalika aliwataka waislam hao wanajitokeza katika mikutano ya Tume ya kuratibu marekebisho ya katiba ambayo imeanza kukusanya maoni ya wananchi mkoani hapa tangu Julai 2 ,waka huu Wilayani Biharamulo.
No comments:
Post a Comment