Waandishi wa
mitandao ya kijamii na tovuti kupewa tuzo kutokana na jitihada na mafanikio
yao.
Tuzo hizo
kuitwa “ Tuzo za umahiri wa digitali za Vodacom”
Kampuni ya
simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa waandishi bora kumi mahiri
katika mitandao ya kijamii kutokana na umahiri wao.
Tuzo hizo
ambazo zimepewa jina la “Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom”, zitatolewa kwa
washindi kumi kutokana na jitihada zao na mafanikio yao ikiwa ni kwa mala ya
Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za Mkononi ya Vodacom.
Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa Waandishi wa
mitandao ya kijamii wanao mchango mkubwa katika kutoa taarifa mbalimbali ndani
ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa.
Wapo waandishi
wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala mbalimbali kuhusu
biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja, Ni kwa sababu hii ndio
maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana na mabadiliko waliochangia
katika utoaji wa taarifa” Alisema Meza.
Baadhi ya sifa
ambazo zitapewa kipaumbele katika tuzo hizi, pamoja na mambo mengine, ni ubunifu
na utoaji wa taarifa za kijamii, Kuzingatia ueledi wa uandishi na uhuru wa
vyombo vya habari, mahusiano na wasomaji katika utoaji wa taarifa, umahiri wa
picha na ushirikishwaji wa vyombo vingingine.
Waandishi wa
mitandao ya kijamii wata shindanishwa kadri inavyowezekana ili kuwawezesha
kuongeza ueledi na umahiri katika kazi zao.
Kampuni ya
Vodacom Tanzania pia itaanzisha mfuko wa fedha wa maendeleo ya digitali, Kwa
mujibu wa Meza fedha hizi zitatumika katika kuendeleza umahiri na kuboresha kazi
katika mitandao ya kijamii na tovuti.“Huu ni mchango kutoka Mfuko wa M-pesa
ambapo waombaji wataweza kuzitumia katika udhamini na kuendeleza shughuli zao”,
Alisema Meza na kuongeza kuwa, “ Tunathamini mchango wa kila mtu, na tunahitaji
waandishi wa mitandao ya kijamii wote waendelee kufanya kazi zao nasi
tutaendelea kuthamini na kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”
No comments:
Post a Comment