Monday, July 29, 2013

Wanaomezea mate maeneo ya ardhi ya JWTZ waonywa



Na Theonestina Juma,Missenyi
SERIKALI imetoa angalizo kwa wananchi wake wanaotamani maeneo ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) kamwe hawawezi kuruhusiwa kutokana na maeneo hayo ni kwa ajili ya usalama wa nchi.
Angalizo hiyo imetolewa jana na Rais Jakaya Kikwete wakati
akihutubia wananchi katika uwanja wa mashujaa Bunazi ambao ulitumika kuwapokelea wapiganaji kutoka vita vya Idd Amin mwaka 1979 wilayani Missenyi.
"Kuna watu wanamezea mate maeneo ya JWT hapa nchini lakini
kamwe hawawezi kuondoka, labda mpaka nipewe taarifa na kujiridhisha, kwani hakuna nchi ambayo Jeshi haina maeneo yake maalum kwa kazi maalum”alisema Rais Kikwete.
"Watu wasidhani kuwa wanaotamani ardhi ya Tanzania waliishia
kwa Idd Amin pekee, wako wengi hadi hivi sasa kwani hata marafiki zako iko siku wanaweza kukugeuka tu"aliongeza.
Rais Kikwete alisema watu wasidhani kuwa  maeneo wanakokaa wanajeshi wanakaa tu, bali ni kwa ajili ya kazi maalum ya kulinda usalama wa nchi na wananchi.
Alisema kamwe wananchi wasitegemee kuwa maeneo ya mipakani jeshi linaweza kukaa nyuma ya mlima hiyo haiwezekani wenyewe wanautaratibu wao.
Alisema kama kuna tatizo kati ya wananchi na JWTZ heri waambiwe kwanza na Mbunge kabla ya kuwafikishia wananchi.
Alisema kabla ya kutoa maamuzi kwanza atahitaji taarifa kamili juu ya ardhi ya wapi katika eneo gani wanayohitaji wananchi.
Alisema " wanajeshi kuondolewa katika maeneo hayo huenda ni kuwapunguzia usalama wa nchi"
 Maelezo hayo yaliojaa angalizo ya Rais yalitokana na malalamiko ya wananchi wa Jimbo la Nkenge kwa Mbunge wao Assumpta Mshama ambaye nae aliyawasilisha kwa Rais.
Bi.Mshama alisema kuna maeneo ya ardhi ya wananchi ambayo yamechukukiwa na Jeshi na kukaa bila matumizi yoyote.

No comments:

Post a Comment