Monday, July 29, 2013

Rais Kikwete amsafisha Waziri Magufuli katika sakata la kujipendelea kujenga barabara nzuri jimboni kwake kabla ya Biharamulo



Na Theonestina Juma, Biharamulo
SERIKALI imewataka makampuni Wakandarasi wa hapa nchini kuiga mfano wa wakandarasi wa barabara ya Kampuni ya CHICCO kwa kufanya kazi nzuri na kujisimamia na kujindesha wenyewe licha ya serikali kutokamilisha malipo yao kwa wakati.
Rais Jakaya Kikwete amesema hayo  jana katika hafla fupi
ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Kagoma Lusahunga wenye
urefu wa kilomita 154 iliofanyika wilayani Biharamulo
Alisema Kampuni hiyo imejenga barabara ya Lusahunga hadi Kagoma kwa muda mfupi ambapo hadi sasa bado wanaidai serikali sh.bilion 40 ambayo watalipwa muda si mrefu.
Alisema lengo la serikali kukazania ujenzi wa barabara ni mkakati mpango wa kufungua nchi ili iweze kupitika kwa mikoa yote ya hapa nchini kuunganishwa kwa lami  licha hadi 2015 hatakamilisha labda kwa Rais ajaye.
Alisema licha ya barabara hiyo kuiwekea jiwe la msingi lakini
ukweli ni kuwa ujenzi wa barabara hiyo imeshakamilika ambapo imebakia mita 500 tu kukamilika.
Kuhusu manung'uniko kuwa Waziri wa Ujenzi, John Mafugufuli kuwa anajipendelea kwa kujengea bara bara ya lami ya Chato Buzirayombo si kweli bali ilikuwa ni mpango wa serikali.
”Si kweli kuwa Dkt.Magufuli alijipendelea kujengwa barabara hiyo kabla ya Kagoma Lusahunga bali ulikuwa ni mpango wa serikali”alisema.
Hata hivyo, Rais Kikwete amewataka wananchi kulinda na kutunza bara bara zinazojengwa ili ziweze kudumu kwani serikali inatumia pesa nyingi katika barabara.
"Kitu kikubwa ni kutunza barabara wapo maadui yake kama mvua
na matendo ya wanadamu kuzidisha uzito kwenye magari yao, kuchimba mchanga kando kando ya barabara, kumwaga oil,na ndiyo sababu kila barabara wameweka mzani"alisema.
Naye Waziri wa Ujenzi John Magufuli akizungumza katika hafla hiyo alisema hajawahi kumpongeza mkandarasi yeyote yote lakini kulingana na utendaji kazi wa wanapaswa kupewa pongezi.
Kwa upande waMtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini,
Bw.Aaron Mfugale alisema ujenzi wa barabara hiyo upembuzi yakinifu
ulianza mwaka 1995 ambapo 2003 alipatikana mkandarasi na kutimuliwa kazi kutokana na uwezo mdogo na baadaye ilipatikana Kampuni ya Chicco waliojenga barabara hiyo kwa miezi 36 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Alisema jumla ya fedha zinazotumika katika mradi huo unaofadhiliwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 ni sh.bilioni 191.

No comments:

Post a Comment