Monday, July 29, 2013

Kikwete:Nchi iko tayari wakati wote, muda wowote



Na Theonestina Juma,Kagera
AMIRI Jeshi Mkuu Jakaya Kikwete  amesema Tanzania haiko
tayari kuchezewa na nchi yoyote ile na kuwa nchi iko tayari kwa saa yoyote, muda wowote kutonana na kulinda usalama wa nchi inagharama
yake.
Rais Kikwete amesema hayo wakati akizungumza na mamia ya wakazi
wa Muleba waliohuria katika maadhimisho ya kumbu kumbu ya mashujaa619 yaliofanyika katika makaburi ya Kaboya wilayani hapa.
"Msiwe na wasi wasi nchi iko imara kijeshi, kiusalama, tutahakikisha tuna kuwa machomuda wowote,saa yoyote, tunawajibu wa kulinda nchi yetu, hatutamruhusu mtu yeyote kuchezea nchi yetu,tuatamfanya kama tulivyofanya kwa Idd Amin"alisema.
Na kuongoza" Wakazi wa Kagera mnajua vizuri yaliotokea ya mwaka 1979,mnajua maisha yalivyoku, hivyo wasiwe na shaka kwani
serikali haitathubutu kumruhusu mtu kuchezea ardhi yake wala kumega
nusu sentimita ya nchi hii".
 Alisema Tanzania haina nchi nyingine pa kukimbilia hivyo watailinda na kutetea na hatairuhusu mtu yeyote aichezee, wala kuimega kwa sababu yoyote ile, kwa mantiki hiyo hawatasita kumshughulikia atakayekuwa na nia kama hiyo.
Alisema chanzo cha yote hayo ni kutokana na Amin kudai kuwa eneo lote la Mtukula hadi mto Kagera ni sehemu ya Uganda hadi eneo hilo alitangaza kuwa niwilaya  mpya ya Rakai  ambapo alitakiwa kuondoka na kukaidi na hivyo hakukuwa jawabu lingine isipokuwa kumwondoa kwa nguvu,kazi ilifanyika na kukomboa mipaka yetu.
"Lakini wakati wao wakivamia waliharibu rasilimali zetu,amri ya Amiri Jeshi wa wakati huo naye alisema kuwa na wao licha ya kukomboa mipaka na hivyo wao walilazimika kusonga zaidi ili nao wapate uchungu wagharama ya kujenga kama sisi, na hii ndiyo maana ya Mbarara”.
Alisema kuna watu waliolipa gharama kwa kutoa maisha yao kwa ajili ya kukomboa Watanzania ambao ndiyo hao mashujaa 619 waliolala katika makaburi ya Kaboya.
Alisema kutokana na hali hiyo serikali itaendelea kuwahudumia
mashujaa waliotoa uhai yao kwa ajili ya kukomboa wananchi ili kuondoa malalamiko yaliopo ya kichini chini kuwa serikali imewasahau mashujaa hao kwani wapo ambao walipata ulemavu wa maisha.
Alisema kinachotakiwa ni Maofisa wa Jeshi kuieleza serikali ifanye nini kwa ajili ya mashujaa hao waliokuhani maisha yao,kwani walijitolea mhanga kukomboa nchi yetu.
Kamwe serikali haiwezi kuwasahau mashujaa wetu,kazi kwao
wanajeshi, kitu ambacho hakijafanyika niambieni, tuifanye,ili
ijulikane kuwa watu hawa walijitolea kwa ajili yetu,kwani wapo wale
ambao wako hai na baadhi ya viungo vyao havifanyi kazi hao tutaendelea kuwahudumia"alisema.
Alisema kulinda nchi ni kazi ngumu , kutetea taifa ni kazi ngumu,na kuna wakati unalazimika kufanya hivyo,kwa maisha yako
kama walivyofanya hao mashujaa waliolala hapo.
Awali Rais Kikwete alipomtaka Mkuu wa Majeshi Davis Mwamnyange kuwaeleza wananchi juu ya usalama wa nchi,alisema kuwa jeshi liko imara muda wote na wala wananchi wasiwe na wasi wasi kwani wako macho.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini,Charles Mwijage alimweleza Rais Kikwete kuwa wananchi wa maeneo hayo hawana mahusiano mazuri ya mipaka hivyo wananchi hao wanatakiwa kuelezwa mipaka.
"Wananchi hawana mahusiano mazuri kambi la Kaboya hivyo wanatakiwa wawekewe mipaka ili ijulikane kwani wewe ndiye msuluhishi wa mambo yote"alisema.
Hata hivyo Rais Kikwete alimwagiza Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka kukaa na uongozi wa kambi ya Kaboya na viongozi wa wananchi ili wajadili tatizo hilo na kupatiwa ufumbuzi.



Katika maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi, viongozi wa dini, serikali,vyama vya siasa, mawaziri, Rais wa Zanzibar, Dkt.Mohamed Shein na Makamu wa Rais, Dkt.Ghalib Bilal.mwisho

No comments:

Post a Comment