Monday, July 29, 2013

Nimechoka, JWT kufanya operesheni kuwasaka wahamiaji haramu na majambazi



Na Theonestina Juma, Biharamulo
 AMIRI Jeshi Mkuu,Rais Jakaya Kikwete amewatangazia kihama Majambazi, wanaomiki silaha kinyume cha sheria na wahamiaji haramu kujisalimisha na kusalimisha silaha zao ndani ya wiki mbili, baada ya hapo watakumbwa na msako mkali ambao haujawahi kutokea nchi hii.
Rais Kikwete ametoa agizo hilo jana katika hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Kagoma Lusahunga yenye urefu wa kilomita 154 iliofanyika wilayani Biharamulo.
"Nimechoka, Watanzania hawawezi kuwa watumwa ndani ya nchi yao, wakitaka kusafiri hadi magari yao yasindikizwe na askari wenye
silaha... maisha haya mpaka lini, ninataka Watanzaia waishi kwa raha zao na sitaki ugomvi na chi jirani"alisema.
Alisema Majambazi, wahamiaji haramu na wanaomiliki silaha kinyume cha sheria anawapatia wiki mbili kujisalimisha baada ya hapo watasakwa kila sehemu za mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma hadi ndani ya nyumba zao wanakojificha kwa kutumia majeshi yote ya usalama.
"Upuuzi huo hatuuwezi kukubali, watu hao tutawasaka ndani ya nyumba zao,kwenye handaki wanakochimbia sialaha zao, kama ni wahamiaji haramu kutoka nchi jirani waondoke,warudi makwao, katika hili stanii...majeshi yote ya usalama, likiwemo Jeshi la wananchi na usalama wa taifa"alisema.
Nasema haya kwa macho makavu na mchana kweupe, na ole wao kwa wale watakao jaribu kuwafyatulia askari wetu risasi jeshi limkamate mateka nadhani nikisema hivyo kwa lugha ya kijeshi mnaelewa" alisisiza Rais Kikwete huku akishangiliwa na wananchi waliofurika kumsiliza.
Aidha Rais Kikwete ametoa tahadhari kwa Watanzania wanaojua wanaowahifadhi na kushirikiana na majambazi na wahamiaji haramu kuacha mara moja na watafute shughuli ya kufanya.
Alisema katika msako huo utakaoshirikisha JWT hakuna cha msalia mtume kwani tayari tumeshawapatia muda wa kuondoka hapa nchini.
Alisema kwa mhamiaji haramu anayetaka kuishi nchini heri afuate utaratibu wa kuingia na kusihi nchini lakini si vinginevyo.
Alisema tayari ameshatoa taarifa kwa vyombo vyote vya usalama kazi kwao kuanza utekelezaji baada ya wiki mbili kupita.

No comments:

Post a Comment