Monday, July 29, 2013

Rais Kikwete ahadi yangu bado iko pale pale

Na Theonestina Juma,Kagera RAIS Jakaya Kikwete ameweka jiwe la msingi
katika upanuzi wa uwanja wa ndege ambao kuja kukamilika kwake
utagharimu zaidi ya sh.bilioni 21

, Rais Kikwete alisema ni
mmoja wa kutimiza ahadi yake ya mwaka 2010.
"Ahadi yake bado iko pale
pale huu, tunaita kuwa ni ukarabati  lakini mpango wetu wa kujenga
kiwanja cha kimataifa katika eneo la Omukajunguti Wilayani
Missenyi"alisema.Alisema kujengwa kwa kiwanja hicho kitawezesha kutua
ndege kubwa na kupunguza tatizo lililopo.
Awali  Waziri wa Uchukuzi,
Dkt.Harson Mwakyembe akimkaribisha Rais kuweka jiwe la msingi alisema
kuwa ili kuimarisha usafiri wa anga Wizara itaendelea kusimamia sera
ya taifa ya uchukuzi na kuiboresha kika mara ili sekta hiyo iweze
kuchangia katika pato la taifa na kukidhi matarajio ya wadau wake na
kwamba viwanja vyote vya ndege vya mikoa kama Mara,Mtwara, Lindi
vitaendelea kuboreshwa.
Naye  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi
akisoma Taarifa yake Mhandisi John Mngodo mradi huo wa ukarabati na
upanuzi wa uwanja huo ni miongoni mwa miradi inayogharamiwa kwa mkopo
kutoka benki ya dunia pamoja na fedha za serikali ya Tanzania.Alisema
ili kukamilika kwa ukarabati huo jumla ya sh.bilioni 21.015 zitatumika
ambapo jengo la abiria litaweza kuhudumia abira 500, 000 kwa
mwaka.Alisema ukarabati huo wa mjini hapa unafanywa na Mkandarasi
MECCO ya Tanzania ikishirikiana na CGG ya Italia na kusimamiwa na
Mhandisi Mshauri SSI Engineers and Environmental Consultant
(PTY)kutoka Afrika Kusini kwa ushirikiano na Kampuni za Howard
Humphreys na Nosuto Associates za  Tanzania na Netherlands Airports
Consultants ya Uholanzi kwa gharama ya sh. Bilioni 4.6 ambapo hiyo ni
kwa usimamizi wa viwanja vya Tabora, Bukoba na Kigoma.Alisema mradi
huo ulianza rasmi Februari mwaka jana na unatarajiwa kukamilika
Frebruari mwakani
.

No comments:

Post a Comment