Na Theonestina Juma,Kagera
ULEGEVU wa Maofisa wa Idara ya uhamiaji
nchini hasa maeneo ya mipakani chanzo cha wahamiaji haramu kufikia
zaidi ya 56,000 kutokana na kujua bei zao ndogo, jambo ambalo ni tishio
na hatari kwa usalama wanchi kwa miaka 50 ijayo.
Kauli hiyo
imetolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati wa majumusisho ya ziara yake ya
siku sita mkoani hapa, uliofanyika katika Ikulu ndogo katika Manispaa ya
Bukoba na kuhudhuriwa na wakuu wote wa Wilaya, wakurugenzi, baadhi ya
watumishi wa serikali ,sekta binfasi na viongozi wa dini.
Alisema “
ulegevu wa maofisa wa idara ya uhamiaji haramu ya kutokuwa wafuatiliaji
, wao ni chanzo na sehemu ya tatizo, kwani pindi watu hao wanapoingia
hakuna anayewafuatilia na kuwauliza wameingije nchini, kibali kiko
wapi, matokeo yake wahamiaji haramu wanaingia nchini kwa kasi ya ajabu
jambo linatolishia usalama wa nchini miaka 50 ijayo”.
Alisema maofisa
hao wanatakiwa kusimamia kikamilifu utambuzi wa watu wasio raia na
kufuatilia vitabu walivyopeleka maeneo ya vijijini, kata na tarafa.
“Kuna
watu wanaishi nchi hii kwa kibali cha mtendaji wa kijiji, Afisa
mtendaji wa kata, kwa kuhongwa ng’ombe wawili, lakini kwa afisa uhamiaji
makini lazima amfutilie Yule mtu na kumuuliza umeingiaje humu,
akimwonesha kibali cha mtendaji awakamate na kuwapeleka wote mahakamani
kwani wanakuwa wameingilia kazi ya Idara ya uhamiaji…, tatizo wameachwa
muda mrefu, wamezoea”alisema.
“Maofisa hawa wa uhamiaji, ndiyo
wameifikisha nchi hapa tuliko jambo kubwa wao wanalifanya ovyo ovyo tu,
pale wanapotakiwa kuchua hatua hawachukui kwa nini, viongozi wenu
wanafanya mchezo na wahamiaji haramu ambao miaka 50 ijayo wataambia
wenyeji kuwa ni wageni na wao kuonekana kuwa ndiyo wenyeji, hili ni
jambo ambalo haliwezekani hata kidogo”aliongea kwa kuhamaki.
Aidha
alionesha kushangazwa na uchunguzi zinazofanywa na Taasisi ya kupambana
na rushwa pamoja na maofisa wa Idara ya uhamiaji licha ya kuwepo kwa
saini ya mtendaji wa kijiji, kata, ama diwani kwenye kibali
wanachowapa wahamiaji haramu, lakini huchukua muda mrefu katika
uchunguzi bila kuangalia kuwa uingizaji watu nchini kinyume cha
utaratibu ni tatizo.
Lazima suala la wahamiaji haramu kutazamwa kwa
jicho la kipee si kwamba hatutaki waishi nchini la hasha bali wafuate
utaratibu wa kuingia na kuishi nchini.
Rais Kikwete alisema kila
wilaya na vituo alikolazimika kusimama kuwasikiliza wananchi kilio cha
kwanza kilikuwa ni juu ya wahamiaji haramu.
Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa wilayani Missenyi
Kwa sasa watu
wananung’unikia lakini huko mbeleni litakuwa tatizo kumbukeni, labda
mimi sitakuwepo, lakini kwa kizazi hicho kijacho, watamlalamikia nani,
si sisi ndiyo chanzo cha haya yote kwa nini tusichukue hatua mara moja
kutokomeza jambo hili, kwa nini suala kubwa tunalikukuliwa kwa uzito
mdogo?alihoji.
Alisema uongozi wa Mkoa wa Kagera unapaswa kujua kuwa
watu hao sio ng’ombe wanaoswagwa hivyo katika utaratibu unatakiwa
kufuata unaostahili wa kuwaondoa hapa nchini ikiwa ni kujulishwa .Alisema
“Katika suala hili la wahamiaji haramu, msako sio jibu akiingia nchini
akiingia nchini aondoke kwani serikali kupata sh. milioni 800 kwa ajili
ya shughuli hilo pia ni tatizo kubwa”.
Alisema baadhi ya wahamiaji
haramu hao wanajiita ni Watanzania lakini cha kusitikisha na kushangaza
ni kuwa hawajui hata kuzungumza kiswali jambo linalosikitisha .
Halidhalika Rais Kikwete alisema kuwa chanzo cha kuharibika kwa usalama
kwa upande wa Kagera ni kutokana na kuingia kwa wakimbizi hapa nchini
ambapo mwaka 1963 walikuwa ni wa aina nyingine ambapo tena walioingia
mwaka 1993 waliingia nchini na bunduki zao.
“Miongoni mwa hao
wakimbizi wapo waliojisalimisha na wengine walijificha na sialaha zao
kwa ajili ya kufanyia uhalifu, pori la kimisi na burigi wanyama
wamekwisha , wakimbizi waliwamaliza, watu hao wameacha sihala nzito na
ndogo ndogo tunataka tuziondoe”alisema.
Alisema wanatakiwa kuondoa
mifugo yanayochungwa katika mapori hayo ili hifadhi ya wanyama ibaki
kwa ajili wanyama pekee na sio mifungo ambao wamesababisha baadhi ya
wanyama pori kukimbia.
Alisema wakati wa Hayati Mwalimu Julias
Nyerere walipotakiwa kuchukua uraia ni wakimbizi 30,000 tu ndiyo
waliochukua uraia wengine walikataa, na wakati wake huu ni
wakimbizi 160,000 ndiyo waliochukua uraia.
Alisema si kwamba hawataki
watu kuchukua uraia na kuukana uraia wanchi yao la hasha bali wafuate
utaratibu na nchi wasiibalidi kama shamba la bibi ya kila mtu anaingia na kutoka jinsi anavyojisikia.
No comments:
Post a Comment