Monday, July 29, 2013

Serikali kupambana na wanaokwamisha miradi ya ujenzi wa barabara nchini

 Sehemu ya wanafunzi waliohudhuria katika hafla ya uwekeji jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Bugene Kyaka.
 Rais Kikwete akiweka jiwe la msingi.

Na Theonestina Juma,Karagwe
SERIKALI imesema haitawaruhu baadhi ya watu wachache kuzuia utekelazaji wa miradi mbali mbali kama za  kuunganisha kwa lami  mitandao ya barabara zake hapa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Rais Jakaya Kikwete wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Kyaka Bugene yenye urefu wa kilomita54.1.
"Serikali itatumia mamlaka yake kupambana na baadhi ya watu wanaokwamisha maendeleo ya wananchi"alisema.
Aidha Rais Kikwete alimwagiza Waziri wa Ujenzi, John Magufuli kuendelea na mipango yake ya ujenzi wa barabara kwa maendeleo ya wananchi.
Rais Kikwete alisema dhamira ya serikali kuweka mkazo wake katika ujenzi wa barabara ni kutaka njia kuu za mikoa kuunganishwa kwa lami.
Awali Wazira wa Ujenzi, Dkt.Magufuli alimwomba Rais Kikwete aweze kumruhusu kuwasimamisha kazi baadhi ya wasimamizi washauri wa makandarasi wa barabara ili wasifanye nchi ya Tanzania ni kama sehemu pa kuchotea hela.
"Mheshimiwa Rais, naomba kwa ruhusa yako tuzidi kuwafukuza na
kuwa simamisha kazi baadhi ya wasimamizi washauri wanaoshindwa
kuwasimamia kikamilifu makandarasi wa barabara na kufanya Tanzania
kama sehemu pa kuchota hela"alisema.
Alisema katika ujenzi wa barabara ya Kyaka Bugene wasimamizi Washauri ya Kampuni ya Sai kutoka India na kwa kushirikiana na Kampuni ya Data walifukuzwa kazi Januari mwaka huu tayari wakiwa wameshalipwa sh.bilioni 1.9.
Alisema kwa sasa ujenzi wa barabara hiyo inasimamiwa na Wasimamizi washauri zaidi ya saba wote kutoka makao makuu ya wakala wa barabara nchini.
Hata hivyo alisema katika ujenzi huo wa barabara watu zaidi ya 400 tayari wameshalipwa fidia zao isipokuwa watu wane wakiongozwa na mtu mmoja aliyemtaja kuwa Bw.Nehemia Kazimoto ambaye amekataa kupokea zaidi ya sh.milioni 100 kwa madai kuwa ni kiasi kidogo.
"Bwana Kazimoto,wewe ni Kazimoto, mimi ni 'moto kazi' nyumba
zako zitabomolewa, na kama hutaki kuchuku fidia yako uende mahakamani, tunaheshimu uhuru wa mahakama lakini tutaendelea na kazi yetu"alisema.
Awali Mtendaji Mkuu wa Wakala wa barabara Taifa, Mhandisi
Aaron Mfugale barabara ya Kyaka Bugene inajengwa na Kampuni ya Chicco kwa gharama ya sh.bilioni 64.61 ambapo muda wa utekelezaji wake ni miezi 27 na hatua ya ujenzi wake imefikia asilimia 38.
 Alisema upembuzi yakinifu ya ujenzi wa barabara hiyo ilianza ilianza Novemba 2009 kwa sh. Milioni 386.6 kwa miezi sita kwa kuzingatia vigezo mbalimbali.
Alisema jumla ya sh.bilioni 21 ameshalipwa mkandarasi na
zaidi ya sh.bilioni 2.888 zimelipwa watu kama fidia.





Rais Kikwete akiongoza viongozi mbali mbali kukata utepe sehemu ya mitambo inayotumika katika ujenzi wa barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment