NaTheonestina Juma, Karagwe
RAIS Jakaya Kikwete amesema ole wao wenyeviti wa vijiji, maofisa watendaji wa kata, vitongoji na madiwani wanaojifanya mawakala wa maofisa wahamiaji wanaotoa vibali kwa wahamiaji haramu watakaobainika watakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Onyo hilo limetolewa na jana na Rais Kikwete kwa nyakati tofauti katika wilaya za Kyerwa na Karagwe wakati akizungumza na wananchi.
“Masuala ya Uhamiaji haramu imeshatuchosha na hali hii inatokana na baadhi yenu nyie wananchi kuwapokea na kuwapatia hifadhi na kuna baadhi ya wenyeviti wa mitaa,vijiji kata na madiwani wanaojifanya mawakala wa maofisa uhamiaji wanatoa
vibali kwa wahamiaji haramu, ndani ya wiki wiki zijazo tutaendesha msako mkubwa
wa kuwasaka na wale watakaobainika watakamatwa na kufishwa mahakamani”alisema
Alisema wahamiaji hao wanapopewa vibali hivyo huvidurufu na kugawiana na hivyo huanza
kuingiza mifugo nchini kinyume cha sheria.
“Jana nimepita katika pori la kimisi wakati tunaenda wilayani Ngara, katikati ya pori niliona ndama bila mama yake hivi inawezekaje ndama kuwa peke yake, nikamuuliza Mkuu wenu wa Mkoa, Kanali Fabian massawe ananiambia kuwa ni ya wahamaji haramu, wanaingiaje nyie ndiyo mnaowapatia hifadhi halafu mnakuwa wa kwanza kulalamika’alisema
Hivi inakuwaje afisa mtendaji wa kijiji anakuwa afisa uhamiaji kutoa vibali kwa wahamiaji
haramu, kazi ya kumpa mtu aliyetoka nchi
nyingine ni kazi ya Afisa uhamiaji.
Hata wale wahamiaji haramu ambao hawajakamilisha utaratibu wao tutawaondoa halikadhalika
wale Maafisa uhamiaji ambao hawatekelezi jukumu lao nao tutwashughulikia.
Kauli hiyo ya Rais Kikwete kwa siku ya jana ilitokana na baada yaMbunge wa Jimbo la Karagwe, Gozbert Blandes kumwomba Rais Kikwete anawaidie namna ya kuwaondoa wahahamiaji haramu ambao wamekuwa kero kubwa wananchi wa wilaya hiyo.
Rais Kikwete alisema uondoaji wa wahamiaji haramu utaenda sambamba na zoezi la kuwasaka wale wote wanaomiliki silaha ya kinyume na sheria ambazo mara nyingi hutumika kutekeleza vitendo vya uharifu katika mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma
litakaloendeshwa na jeshi la polisi, la wananchi na idara ya usalama wa taifa baada yawiki mbili kuanzia jana Julai 26,2013.
Alisema kuwa hatakubaliana na maofisa wa serikali wasio waaminifu katika kutekeleza wajibu
wao, “nimeelezwa tabia ya baadhi ya viongozi ya kupokea rushwa ya ng’ombe na
fedha na baadae kutoa vibali kwa wageni vya kuishi nchini,” sasa natangaza vita dhidi ya watendaji wa serikali wanaofanya kazi kinyume na maadili, nitawashughulikia kikamilifu, wenye tabia hiyo
nawashauri waache mara moja” alisisitiza
Rais Kikwete alisema wahamiaji haramu hasa wanaoingia nchini na mifugo wanaleta madhara
makubwa kwa kuwa wanachangia uharibifu wa mazingira, alisema wanajihusha na
biashara ya uchomaji mkaa na ukataji wa miti kwa ajili ya kujenga makazi yao.
Alisema wale wanaojijua kuwa ni wahamiaji haramu waondoke, kwani Watanzania hawataki ugovi na jirani zao.
No comments:
Post a Comment