Na Theonestina
Juma, Kagera
WANANCHI wametakiwa kuchangamkia fursa ya umeme mara ifikapo katika
maeneo yao kwa kuingiziwa ndani ya
nyumba zao kwa ajili ya kuchochea maendeleo yao.
Rai hiyo imetolewa
na Rais Jakaya Kikwete kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi Kata
ya Nyaishozi Wilayani Karagwe na Manispaa ya Bukoba.
Rais Kikwete
alisema serikali imepanga kuongeza uzalishaji
wa nishati ya umeme na kufikia megawati 3,000 ifikapo mwaka 2015.
Alisema
katika mpango huo pia itaiunganisha katika grid ya taifa mikoa yote nchini ili
kuharakisha maendeleo ya wananchi ikiwemo maeneo ya vijijini.
Alisema “
umeme wa grid ya taifa ndiyo tunaupa kipaumbele, kwa vile ndiyo kitakuwa kichocheo
cha maendeleo kwa wananchi”alisema.
“Umeme wa Uganda
hautoshi, kwani hata Waganda wenyewe
umeme huo hauwatoshi, huo umeme si kwa ajili ya uzalishaji kulingana na jinsi
ulivyo”aliongeza.
Alisema mpango
wa kuongeza uzalishaji wa umeme unakwenda pamoja na kuongeza uwezo wa kuusambaza na kuunganisha mikoa ambayo
haikuwa katika grid ya taifa.
Alitaja
mikoa hiyo kuwa ni pamoja na Kagera,Mtwara, Ruvuma ,Lindi, Katavi, Ruvuma,Rukwa,
na kigoma.
Hata hivyo
Rais Kikwete aliwageukiwa Maofisa wa TANESCO na ksuema kuwa wanatakiwa kutambuwa
kuwa wanaishi kwa kuuza umeme hivyo tabia ya kuwaringia wananchi pindi
wanapotaka waunganishiwe nishati hiyo ndani ya nyumba zao waache.
“Kuna baadhi
ya maofisa wa Tanesco wananchi wakihitaji waingizie umeme ndani ya nyumba zao,
wanataka mpaka wabembelezwe, wahongwe … ofisa heshima yako inapungua kwa tabia
hiyo”alisema Rais kwete.
Katika hatua
nyingine Rais Kikwete aliwataka wananchi wanapokuwa wakidai haki yao lazima nao
watimize wajibu wao wa kuunganishwa
nishati hiyo katika nyumba zao.
Halikadhalika
alisema wananchi hao wakiwa hodari kudai nao wawe hodari katika utekelezaji ili
uwekezaji wa nishati hiyo ilingane na usambazaji na uunganishaji.
Aidha kwa upande wa Waziri wa Nishati na madini, Profesa
Sospeter Muhongo alisema bajeti ya wizara hiyo imeongeza kutoka sh. bilioni 600
hadi kufikia trioni 1.2.
Alisema kwa
sasa serikali ina mpango wa kuachana na umeme wa mitambo ya mafuta kutokana na
gharama kubwa ya uendeshaji ambapo
serikali imepanga kuongeza kasi ya kupeleka umeme maeneo ya vijijini.
Hata hivyo,
Profesa Muhongo aliwataka madiwani nchini kupunguza safari za halmashauri ili fedha
zipatikane za kuunganisha umeme wa jua katika maeneo ya shule za sekondari
nchini kupitia wakala wa umeme vijijini [REA]..
“Umeme wa
jua kuunganishwa katika shule moja ya sekondari katika vyumba vinane gharama yake sh. milioni 3.9, ni kiasi kidogo
sana, shule za sekondari hasa maeneo ya vijiji wanaweza kuingiziwa umeme wa jua
, kama madiwani watapunguza safari zao ndani ya halmashauri”alisema Profesa
Muhongo.
Alisema halmashauri zinatakiwa kushirikiana na REA kupeleka umeme vijijini, badala ya kubaki kusubiria serikali kuu.