Sunday, August 12, 2012

Zikiwa zimebaki siku 12, Wenyeviti wa mitaa Bukoba watishia kutoshiriki katika zoezi la Sensa


Na Theonestina Juma, Bukoba
WENYEVITI wa Serikali za mitaa katika Manispa ya Bukoba kupitia umoja wao wametishia kutoshiriki katika zoezi la sensa iwapo hawatapewa mafunzo ya namna gani wanavyotakiwa kushiriki katika zoezi hilo Agosti 26, mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa jana na Umoja wa wenyeviti wa serikali za Mitaa katika Manispaa ya Bukoba uliofanyika katika ukumbi wa Bukoba klabu ulioko mjini hapa na kuhudhuriwa na wenyeviti 63 kutoka mitaa 66.
Walisema tangu maandalizi ya zoezi la kuhesabu watu na makazi yaanze mjini hapa hawajapewa hata mafunzo ya kuwaelekeza nini majumukumu yao na kivipi wanavyopaswa kushiriki katika zoezi hilo licha ya vipeperushi vinavyosambazwa vinaonesha wao wanapaswa kushiriki kikamilifu zoezi hilo.
“Hivi tunashiriki vipi, wakati hata mafunzo ya kutoelekeza namna ya kufanya siku hizo hatujapaewa, kama hatutapewa mafunzo na kuelezwa hatma yetu katika zoezi hilo, hatutashiriki tutakaa majumbani na kuhesabiwa kama watu wengine”walisema.
Mwenyekiti wa Umoja huo, Bw. Yusuph  Omary alisema tatizo kubwa kwa wenye viti wa serikali za mitaa ni namna ya uwezeshwaji kwani hadi sasa hawajaelezwa chochote na Mamlaka husika.
Alisema katika maelezo wanayoyasikia kutoka kwa watu ambao wameshapata mafunzo namna ya zoezi hilo litakavyotekelezwa, Makarani ambao ndiyo wahesabuji watatakiwa kuwandamana na wenyeviti wa serikali za mitaa katika zoezi la awali la utambuzi wa kaya na siku yenyewe jambo ambalo hawakotayari kulitekeleza kama hawataambia stahiki zao ziko vipi.
Alisema “hatuwezi kupelekwa mbumbumbu wakati tunachotakiwa kukitekeleza hatukijui,… lazima tuelimishwe”alisisitiza.
Wenyeviti hao walioonekana kukerwa na kutoshirikishwa kikamilifu katika zoezi hilo ambalo waliita kama kunyanyapaliwa na vyombo husika ambapo walisema lazima waelekezwe,nini cha kufanya wakati huo, posho  unakaaje, pia kama mtu ataleta ubishi wao wamfanyeje.
“Hivi kwa sasa tunasikia kuna baadhi ya dini inapinga kuhewabiwa hawa sisi kama wenyeviti tutawajibika vipi kuwapooza ili wakubali kuhesabiwa?
Au wale watakaoleta mambo ya ubishi ubishi wa kutotaka kujibu maswali watakayoulizwa ipaswavyo, kwani tunasikia kuna dodoso ndefu na fupi zilizojaa maswali mengi wananchi wakikataa kuyajibu yotetuwafanyeje, kwani sisi wenyeviti tunaowajua tunatakiwa kuajibika kwao vipi? Walihoji wenyeviti hao.
Hata hivyo, wenyeviti hao walisisitiza kuwa iwapo hawatapewa maelezo juu ya ushiriki wao katika zoezi hilo, hawatashiriki kama wanapovyotakiwa na serikali bali watakaa majumbani ili kuhesabiwa kama raia wengine.
Aidha kwa upande wa mratibu wa zoezi la Sensa katika mkoa Kagera, Bw. Peter Mulinga akizungumzia madai ya Wenyeviti kutoshirikishwa katika mafunzo ya sensa alisema wao hawatapewa mafunzo bali watapewa stahiki zao wakati wa zoezi hilo.
Alisema “hivi Wenye viti wa serikali za mitaa wao wapewe mafunzo ya juu ya nini…kwani wao wajibu wao nini… kazi yao ni uhamasishaji  na kuwa mwenyeji wa karani  wa sensa siku ya zoezi ikifika kazi ambazo hazihitaji mafunzo”.
Bw. Mulinga alisema pamoja na hayo, wenyeviti hao katika zoezi hilo kuna fungu la posho watakayopewa kwa siku hizo na kwamba hakuna mtu atakayeshikiriki katika zoezi hilo bila kupewa posho.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment