Wanamichezo wa mchezo wa Ngumi (Masumbwi) Mkoa wa
Kagera hasa watoto wa kike wenye kipaji cha mchezo huo neema kwao yaja ya
kuendeleza na kuinua vipaji vyao.
Matumaini ya kupata neema hiyo katika Mkoa wa Kagera
imeoneshwa na Mama Zuena ambaye ni Mke wa Kanali Mstaafu Idd Kipingu ambaye ni
Mwakilishi wa Wanawake Maendeleo ya Vijana, Ajira kwa Wachezaji Shirikisho la Ngumi Tanzania.
Mama Kipingu ameamua kutafuta na kuhamasisha vipaji kwa mchezo wa Ngumi (Masumbwi) hasa
hasa kwa akina mama na watoto wa kike walioko shuleni na ameanzia mkoa wa
Kagera baada ya kuambiwa kuwa hapa mkoani anaweza kupata wachezaji wazuri
kutokana na hiostoria ya Mkoa wa Kagera katika Masumbwi.
Baada ya kufika katika Mkoa wa Kagera alikwenda moja
kwa moja katika shule ya Sekondari ya Wasichana ya Rugambwa ili kuuhamasisha
mchezo huo ambapo wanafunzi wa shule hiyo walihamasika sana na mchezo huo na
kuonesha nia ya kujifunza kama watapata vifaa.
Mama Kipingu aliwahakikishia wanafunzi hao kuwa
anatarajia kuwatumia vifaa vya mchezo huo ili kuanza kufunzwa masumbwi na baadae
wapatikane wawakilishi kutoka mkoa wa Kagera na washiriki kitaifa. Pia
alitembelea na Wilaya ya Karagwe na kuhamasisha masumbwi.
Aidha Mama Kipingu alikili kuwa tatizo kubwa katika
michezo ni mikoa kuachwa bila kutembelewa na kutafuta vipaji isipokuwa
wanaangaliwa tu wale walioko Dar es
Salaam na mikoa ya jirani, lakini mikoa mingine inaachwa. “Ili kuondokana na
tatizo hilo tumeamua kuitembelea mikoa na kuhamasisha mchezo huu.” Alisistiza
Mama Kipingu.
Wanamichezo wale wote wanaopenda mchezo wa Masumbwi Mkoa wa Kagera wa Kike na
Kiume wanaombwa kuja kwa Afisa Michezo Katika Mkoa wa Kagera ili watambuliwe
kwa ajili ya kupatiwa vifaa na kuweka utaratibu wa kufundishwa na kufanya
mazoezi ya mchezo huo na watafaidika na ufadhili huo toka Shirikisho la Ngumi
Tanzania.
Imetolewa
na:
Sylvester
Raphael,
Afisa
Habari Mkoa,
KAGERA.
No comments:
Post a Comment