MKUU wa mkoa Kagera, kanali Fabian Massawe ameziagiza
Halmashauri zote za Wilaya mkoani hapa kuhakikisha maonyesho ya mwaka 2013
wanaleta wakulima wengi ili kuweza kujifunza mbinu mpya za teknolojia ya kilimo cha kisasa chenye tija.
Kanali Massawe alitoa kauli hiyo juzi wakati akifunga
manonesho ya Nane Nane yaliofanyika katika viwanja vya Kyakailabwa nje kidogo
ya Manispaa ya Bukoba na kushirikisha halmashauri zote za mkoani hapa.
Alisema kutokana na maonesho hayo ya Nane Nane ni siku ya
maalum nay a kipekee kwa wakulima,halmashauri zinatakiwa kujipanga kikamilifu
kuhakikisha kuwa wanawaleta wakulima wengi pamoja na wafugaji kwa lengo la kuja
kujifunza mbinu mbali mbali za kilimo na ufugaji bora ili kuweza kuongeza tija
kwao na si kuwaleta wachache wanaowachagua wao
.“Naamini kila mkulima anahamu ya kutaka kushiriki katika
maonesho haya, msiwe mnawachagua, waleteni wengi ili nao wajifunze si kuwaleta
wachache kama ninavyohuhudia kwa hi sasa”alisema Kanali Massawe.
Halikadhalika aliiagiza kamati ya maandalizi ya maonesho
hayo kwa mwaka huu mkoani hapa kuanzisha
maonyesho ya mifugo (wanyama) ili na sekta ya mifugo iweze kupata hamasa ya
kutoa elimu kwa wafugaji kujifunza kufuga kisasa kuondokana na ufugaji wa kienyeji
usiokuwa na tija.
Alisema kila mwaka maonesho hayo kwa asilimia kubwa huusisha
wakulima wengi kuliko wafugaji na hivyo kuwanyima fursa yao muhimu.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo aliwataka wananchi
kushiriki katika vikao vya kuibua miradi ya maendeleo katika maeneo yao ambapo
alibainisha kwamba miradi ya kilimo inamilikiwa
na wananchi wenyewe pamoja na Halmashauri za Wilaya.
Pia alitoa wito kwa wakulima kuanza ufugaji wa nyuki ili kujipatia kipato
kutokana na kuuza asali.
“Asali ya mkoa wa
Kagera ni asali bora duniani ambayo ina kiwango cha hali ya juu, pia
kimeanzishwa kiwanda cha kusindika asali mkoani Pwani, fugeni nyuki ina soko
kubwa duniani kote.” aliwasistiza wakulima hao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment