Wednesday, August 22, 2012

Waandishi watakiwa kujijenga ili kuaminiwa na wananchi



 BUKOBA
WAANDISHI wa habari za uchunguzi wametakiwa kujijenga ili kuwezesha watu waweze kuwaamini.
Rai hiyo imetolewa leo na Phil Karashani wakati akitoa mafunzo ya uandishi wa uchunguzi kwa
waandishi wa habari 18 ambao ni wanachama wa Klabu ya waandishi Mkoa Kagera yanayodhaminiwa na umoja wa vilabu vya habari nchini (UTPC).

Karashani alisema ili waandishi wa habari waweze kujijenga lazima waandike taarifa kamili inayosemwa na chanzo na si kumlisha maneno ambayo hajasema.
Halidhakalika alisema waandishi wa habari wanatakiwa kuwa na heshima ili kuweza kuheshimiwa na wananchi.
Kwa upande wa wahariri wa vyombo vya habari wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kuwatuma waandishi wao wanaojiamini pindi viongozi wanapoitisha
mkutano na waandishi wa habari.

"Wakae wakijua kuwa kuna baadhi ya viongozi wanakuwa wameshazoea baadhi ya waandishi na bila kuwepo hawawezi kuanza kuzungumza hadi awaone, hivyo wahariri wanaposikia kuna mkutano na waandishi wa habari wasiwe wanawabadilisha badilisha"alisema.
Alisema licha ya lengo la wahariri ni kutaka kuwajengea uzoefu kwa waandishi wake lakini wanapaswa kuangalia ni katika sehemu gani.
Alisema sababu inayowafanya baadhi ya viongozi kuwapenda baadhi ya waandishi fulani kuhudhuria katika mikutano yao ni kutokana na kuwajua kwa majina ambapo alitoa mfano kama mkutano na waandishi wa habari unapofanyika white house,Marekani,  Hilary Clinton huwaita kwa majina pindi wanapouliza maswali.

No comments:

Post a Comment