Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk.
Steven Ulimboka, jana alirejea nchini kutoka nje ya nchi alikokwenda kutibiwa
baada ya kutekwa na kuteswa vibaya na kisha kutupwa katika msitu wa Pande nje
kidogo ya jijini Dar es Salaam.
Watu wengi wakiwemo madaktari, wanaharakati na wanafamilia walifurika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kumpokea Dk. Ulimboka ambaye tukio lake la kutekwa na kuteswa lilivuta hisia za watu wengi.
Kabla ya kuwasili uwanjani hapo, madaktari, wanaharakati na wananchi, walizingira mlango ambao wasafiri huutumia kutokea, wakisubiri kwa shauku kubwa kumuona.
Wakiwa katika mlango huo walikuwa wakiimba nyimbo huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Baadhi ya ujumbe huo ambao ulikuwa umeanzia na jina la Dk. Ulimboka zinasomeka: ‘Damu yako iliyomwagika ina amsha ari ya wananchi kudai haki ya afya, Karibu nyumbani, uliumizwa kikatili ukitetea haki ya afya bora kwa wananchi wote, tupo nawe pamoja mapambano yanaendelea.'
Nyingine zilisema: Kamwe harakati za kudai haki hazitanyamazishwa, ushujaa wako umezaa nguvu mpya na shujaa mpiganiaji wa haki ya afya bora kwa wananchi.
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu, hatimaye saa 7:50 mchana, Dk. Ulimboka alitoka nje huku akitokwa machozi na ndipo pilikapilika zilipoanza ambapo kila mtu alikuwa akimsukuma mwenzake ili amuone, hali iliyosababisha waandishi wa habari kupata wakati mgumu kufanya kazi yao.
Baadhi ya wanawake walikuwa wakipiga vigelegele, nyimbo zikiimbwa, huku wengine wakisikika wakisema shetani ameshindwa.
Wengine wakikimbia huku na kule hususani waandishi wa habari kwa ajili ya kupata picha ambapo hata hivyo, walikuwa wakizuiwa na umati wa watu na ndipo baadhi ya madaktari walipoamua kumzunguka Dk. Ulimboka kwa ajili ya kumlinda ili apate nafasi ya kuzungumza.
Akizungumza huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa madaktari hao, Dk. Ulimboka alisema anamshukuru Mwenyezi Mungu kumpona hadi kufikia katika hali aliyonayo sasa.
“Moyo wangu umefarijika sana, ninawashukuru sana, ninamshukuru Mwenyezi Mungu ameniponya kabisa, kama mnavyoniona ninatembea, niliondoka siwezi kutembea na ninawathibitishia Watanzania kwamba ninaweza kufanya kazi yoyote,” alisema na kuongeza:
“Nashukuru madaktari kuniwezesha kupata matibabu na ninawashukuru wananchi wote, afya yangu imeimarika kabisa.”
Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo, Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Edwin Chitage, alisema wanashukuru Mungu Dk. Ulimboka amepona na kwamba kupona kwake kumechangiwa na huduma bora ya afya aliyopatiwa nje.
“Hapa nchini watu wengi wanakufa kutokana na huduma mbovu ya afya, Dk. Ulimboka amepona kutokana na huduma bora walizonazo wenzetu,” alisema.
Aidha, Dk. Chitage alisema madai ya madaktari kuhusiana na kuboreshwa sekta ya afya bado yako pal pale.
Kwa upande wao, baadhi ya wanaharakati waliojitokeza kumpokea walisema kupona kwa Dk. Ulimboka, ni ushindi mkubwa kwa sababu aliyotendewa ni mabaya sana.
“Licha ya ukatili aliofanyiwa Dk. Ulimboka, lakini Mungu amemponya, tuko pamoja naye kuendeleza mapambano na tunaomba wahusika wachukuliwe hatua kali,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Usu Mallya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Ananilea Nkya, alisema mateso aliyoyapata Dk. Ulimboka, ni Mungu mwenyewe ndiye aliyemponya na kuahidi kumuunga mkono katika kupigania haki ya Watanzania.
Dk. Ulimboka alitekwa usiku wa kuamkia Juni 27, mwaka huu na watu wasiojulikana, ambapo alipigwa na kujeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika Msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji Dar es Salaam.
Daktari huyo ambaye alikuwa akiratibu mgomo wa madaktari, aliokotwa na msamaria mwema akiwa amefungwa mikono na miguu huku akiwa taabani.
Baada ya kuokotwa na wasamaria wema na kufikishwa katika kituo cha polisi, Dk. Ulimboka aliwahishwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) kwa matibabu na ilielezwa kuwa hali yake haikuwa nzuri ambapo alipelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi hadi aliporejea nchini jana.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment